Wakina mama wakimlaki Mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Nicholaus Ngassa wakati wa ziara yake aliyoifanya jimboni humo mara baada ya vikao vya Bunge la Bajeti kumalizika hivi karibuni, ambayo ilikwenda sanjari na mikutano ya hadhara.
Na Mwandishi Wetu, Igunga
MBUNGE wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Mhe. Nicholaus Ngassa amewaomba
wananchi wa jimbo hilo kutoteteleka kwa
kauli mbalimbali za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu, kuhusu maendeleo
na kuwahakikishia kuwa chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais
Samoa Suluhu Hassan wapo kwenye mikono
salama na waendele kupokea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia
Ilani ya Chaka hicho.
Ngassa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi kwa
nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara aliyofanya katika Vijiji na
Vitongoji vya Kata ya Kinungu.
“Kinungu tumeleta umeme, barabara, maji ya visima ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa shule
zote za sekondari na msingi na sasa mjiandae kupokea maji ya Ziwa Victoria
kupitia mradi unaotekelezwa kwa thamani ya Sh. Bilioni 20 kutoka kwenye tenki linalojengwa Mlima wa
Bulenya.
Watoto wanasoma elimu bure bila
malipo,tumeongeza upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya na
zahanati za vijijini, haya ndio maendeleo tuliyoahidi mwaka 2020 kwenye kampeni
na tunaendelea kutekeleza, ” alisema Ngassa.
Ngassa alisema hayo yote yanatekelezwa chini ya Rais Dk. Samia Suluhu
Hassan ambaye anatoa fedha nyingi nchi mzima kutekeleza miradi mbalimbali ya
maendeleo.
” Binafsi nichukue nafasi ya kipekee kumshukuru Rais Dk.Samia Suluhu
Hassan kwa kazi hii kubwa anayoifanya kwenye jimbo letu, mkoa wetu na Taifa kwa
ujumla nawaomba ndugu zangu kwa iman zetu tuendelee kumuombea kwa Mungu
ampe afya na maisha marefu,”
alisema Ngassa.
Katika
mikutano hiyo Mbunge Ngassa alipata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali na zile
zilizokuwa ndani ya uwezo wake alizitafutia ufumbuzi wa papo kwa papo kwa
kushirikiana na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na zile zilizokuwa nje ya uwezo wake
alisema ataziwasilisha kwa wahusika