Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akiongea katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alielezea mafanikio ambayo yamepatikana tangu Barrick na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga zianze kufanya kazi kwa ubia.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alielezea mafanikio ambayo yamepatikana tangu Barrick na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga zianze kufanya kazi kwa ubia.Wengine pichani kushoto ni Meneja wa Barrick nchini Tanzania,Melkiory Ngido, na kulia ni Naibu Waziri wa madini,Mh.Stephen Kiruswa.Mkutano huo ulifanyika katika mgodi wa North Mara uliopo wilayani Tarime.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda akiongea katika mkutano huo
Mbunge wa Tarime,Mh. Mwita Waitara akiongea wakati wa mkutano huo
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mara pia ilishiriki katika mkutano huo
Maofisa Waandamizi wa Barrick wakifuatilia matukio
Madiwani na watendaji wa vijiji pia walihudhuria
Msimamizi wa hisa za Twiga kutoka Hazina akiongea katika mkutano huo
Watendaji kutoka taasisi mbalimbali za kijamii wakionyesha hundi za msaada wa Dola za Kimarekani 10,000 kila moja zilizotolewa na Rais wa Barrick,Dk. Mark Bristow baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa madini,Mh.Stephen Kiruswa wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Madini,Mh.Stephen Kiruswa akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha dola za kimarekani 10,000 kwa wawakilishi wa taasisi ya Tulikondelei iliyopo Shinyanga,Bi.Bertha Nyawanga na Daniel Samson zilizotolewa na Rais wa Barrick,Dk. Mark Bristow kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na changamoto za kijamii jana.
**
Kampuni ya Madini ya Twiga, ambayo ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Dahabu ya Barrick, imefufua tasnia ya madini ya dhahabu nchini kupitia ubia ambao unafaa kuwa mfano wa kuigwa kwa shughuli kama hizo, hususan katika nchi zinazoendelea, amesema Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow .
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ziara yake nchini , Bristow alisema kuwa mwaka 2019, wakati Barrick ilipochukua jukumu la usimamizi wa migodi ya North Mara na Bulyanhulu – migodi ambayo sasa inaunda mkusanyiko wa maeneo ya Kampuni ya Twiga – yote ilikuwa imeporomoka na kusimamisha shughuli zake kutokana na mzozo kati ya serikali na waendeshaji wa awali wa migodi hiyo.
“Tulitatua mzozo huo na kuanzisha Kampuni ya Twiga kama ubia wa kugawana faida za kiuchumi kwa uwiano wa 50:50 ambao pia Serikali ya Tanzania inao umiliki wa hisa wa 16% katika kila mgodi. Tuliifufua na kuisuka upya migodi hiyo, ambayo sasa, kama kwa ujumla wake, inazalisha dhahabu kwa kiwango cha Daraja la Kwanza; kwa maneno mengine, mgodi wenye hadhi hii ni mzalishaji ambaye anaweza kuzalisha angalau wakia 500,000 za dhahabu kila mwaka kwa zaidi ya miaka 10 kwa gharama zinazokubalika katika tasnia hiyo. Uendeshaji huu wa shughuli umefanikiwa sana kiasi kwamba, tangu Barrick inunue hisa kutoka kwa wanahisa wenye hisa chache, umechangia kiasi cha zaidi ya dola bilioni 2.8 katika uchumi wa Tanzania kupitia kodi, ushuru, magawio, mishahara na malipo kwa wasambazaji wa ndani,” Bristow alisema.
“Muhimu pia, tumeshughulikia masuala ya mazingira, madai ya ardhi na haki za binadamu ambayo yalichafua sifa za migodi hii na kurejesha ukubalifu wao kwa jamii wa kufanya kazi kama mwanajamii muhimu wa jamii hizo. Aidha, tangu kuanzishwa kwake, Kampuni ya Twiga imewekeza zaidi ya dola milioni 12.5 katika miradi ya kihistoria – inayobainishwa kwa ushirikiano na kamati za maendeleo ya jamii (CDC) tulizozianzisha migodini – ili kutoa huduma bora za afya, miundombinu ya elimu, maji ya kunywa na vyanzo mbadala vya mapato. Miongoni mwa miradi hiyo ni mfumo wa umwagiliaji ambao unatarajiwa kuboresha uzalishaji kwa kiasi kikubwa kwa wakulima wapatao 2,356.”
Barrick-Twiga pia imetoa dola milioni 30 kwa ajili ya Programu ya Kusongesha Mbele Mustakabali wa Shule (Future Forward School Programme). Kwa ushirikiano na serikali, programu hii itajenga vyumba vya madarasa vipatavyo 1,090 na miundombinu mingineyo katika shule zipatazo161 nchi nzima, ili kuchukua wanafunzi 49,000 kati ya wanaokadiriwa kufikia 190,000 ambao wataanza masomo yao ya kidato cha tano Julai mwaka huu. Aidha, imeahidi kutoa dola milioni 40 kwa ajili ya kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 73 kutoka Kahama kwenda Kakola.
Kiuendeshaji, Bristow alisema kuwa mkusanyiko huo wa migodi ya Kampuni ya Twiga (Twiga Complex) umeendelea kuwa na utendaji mzuri wa uzalishaji na uko mbioni kufikia mwongozo wake wa uzalishaji wa mwaka huu. Migodi yote miwili inazingatia sana suala la afya na usalama wa wafanyakazi wao, na mwezi Aprili, Mgodi wa Bulyanhulu ulishinda Tuzo ya Mshindi wa Jumla ya Uzingatiaji wa Taratibu za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Tanzania kwa mwaka 2023 katika Kundi la Sekta ya Madini na Mgodi wa North Mara ulikuwa mshindi wa pili.
Ulimwenguni, Barrick inayo sera ya kuweka kipaumbele cha ajira za ndani na, katika Kampuni ya Twiga, sera hii imewezesha kupatikana kwa nguvukazi ambayo ni Watanzania kwa asilimia 96, huku takribani nusu yao wakitoka katika jamii zinazozunguka migodi ya kampuni hiyo.
Bristow alisema kuwa uchimbaji wa kupekecha katika Mgodi wa North Mara unafanikiwa kuchukua nafasi katika hifadhi zilizopungukiwa au kuishiwa na dhahabu kutokana na uchimbaji, na jiwe la kwanza la dhahabu lilichimbwa katika chimbo jipya la mgodi wa Gena katika robo ya mwaka iliyopita. Fursa zaidi za uchimbaji wa kupekecha zimebainiwa katika migodi yote miwili.
“Barrick imedhamiria kupanua uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania kutoka hapa kwenye kituo chetu kikuu. Kwa sasa, tunaunganisha leseni muhimu za utafutaji madini nchini kwa nia ya kupanua hifadhi na rasilimali zetu zilizopo pamoja na kugundua maeneo mapya yenye dhahabu yaliyo na hadhi ya kimataifa,” alisema.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Madini,Mh. Stephen Kiruswa,aliipongeza kampuni ya Barrick kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika tasnia ya madini ambao mbali na kuchangia pato laTaifa pia umenufaisha jamii kupitia miradi ya uwajibikaji wa jamii ambao inaendelea kutekelezwa katika maeneo yanayozunguka migodi yake.
01.
1.
3.
6.
4.
5.
07.
8.
9.
10.
11.</div