Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukiimbwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Julai 10,2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo Julai 10,2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo Julai 10,2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) likipita kwa mwendo wa pole na haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mejeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda ,akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele,akitoa taarifa ya JKT wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyofanyika leo Julai 10,2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali imedhamiria kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwa la kisasa zaidi lenye kuendana na mahitaji ya sasa katika kutimiza majukumu ya malezi ya vijana kuwajenga uzalendo wenye kulithamini taifa, kujitegemea uzalishaji mali na kulitetea Taifa bila hofu.
Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 10,2023 wakati wa Kilele cha maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JKT yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais Dk. Samia amesema msukumo wa kuanzishwa kwa jeshi hilo Julai 1963 ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na vijana wenye utayari wa kulitumikia taifa lao.
“Dhamira ya Serikali ni kuimarisha JKT ili liwe Jeshi la kisasa zaidi linaloendana na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu, mafunzo yanayotolewa na JKT yawasaidie vijana kuwa wazalendo wa kweli wanaothamini utaifa, umoja na mshikamano wa Watanzania na wanaopenda kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kujitolea”, amesema Dkt. Samia.
“Kutokana na umuhimu wa JKT katika kuwaanda vijana, mwaka 1964 wakati akiwahutubia vijana wa JKT kwenye kambi ya Mgulani, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisisitiza kwamba JKT litakuwa lango kuu kwani kila kijana atalazimika kulipita kabla ya kwenda kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbali.
Ameongeza kuwa: “Ndio maana mwaka huu idadi ya vijana waliojiunga JKT wameongezeka na kila mwaka idadi itaendelea kuongezeka tofauti na wale wanaokwenda kwa hiyari.”
Hata hivyo Rais Samia ametoa maagizo kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuandaa mpango mkakati wa kurekebisha makambi yanayohitajika.
“Naelekeza Wizara ya Ulinzi na JKT kuandaa mpango mkakati wa kurekebisha makambi kwenye Jeshi la JKT katika upande wa malezi ya vijana. Aidha, kuliwezesha Shirika la SUMA JKT kupata mikopo ili wazalishe na waweze kurejesha mikopo na shirika liweze kuendelea, na kama ikitakiwa udhamini wa Serikali, tuko tayari kuwezesha SUMA- JKT ili iweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa”.Amesisitiza Rais Dkt. Samia
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe. Innocent Bashungwa, amesema kuwa mafunzo ya JKT ni muhimu na yana mchango wa amani iliyopo nchini na wataendelea kushirikiana na Wizara za kisekta kuboresha mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana wa jeshi hilo ili kupata stadi na maarifa tofauti na ilivyo sasa.
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda,ameishukuru serikali kwa kuendelea kuiwezesha JKT kwa rasilimali watu na fedha ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
“ Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi na JKT, tumeweka mikakati ya kuliboresha na kulifanya Jeshi la Kujenga Taifa kuwa la kisasa zaidi ili liweze kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani”,amesema Mkuu wa Majeshi.
Awali Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa jukumu la jeshi hilo ni malezi ya vijana, uzalishaji mali na ulinzi wa Taifa na tangu kuanzisha kwake Julai 10 mwaka 1963 linatekeleza majumu kwa ufanisi.
Meja Jenerali Mabele ameongeza kuwa, JKT imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kubadilisha fikra za kikoloni kwa vijana waliohudhuria mafunzo yake, kuwajenga vijana katika hali ya umoja, moyo wa kupenda kazi, uadilifu, nidhamu, uelewano bila kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini, jinsia hivyo kudumisha uhuru na amani ya Taifa.
“JKT imefanikiwa kuwa na ongezeko la idadi ya vijana wanaopata mafunzo ya Jeshi hili ambapo mwanzo lilianza na vijana 11 lakini kwa sasa vijana waliopo makambini wanaohudhuria mafunzo kwa mujibu wa Sheria ni 52,000” amesema Meja Jenerali Mabele.
JKT ilianzishwa rasmi Julai 10, 1963, hatua hii ilikuwa ni utekelezaji wa azimio la kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Aprili 19, 1963 chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Nyerere.