Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akicheza na kufurahi pamoja na Watendaji wa Umoja wa Wanawake wanaomiliki Shule na Vyuo vya elimu ya kati Tanzania (TAWOSCO) wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Umoja huo uliofanyika Ukumbi wa Abla Beach Apertment Kibweni Mjini Unguja,
Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wanaomiliki Shule na Vyuo vya elimu ya kati Tanzania (TAWOSCO) Mercy Sila akisoma Risala ya umoja huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Ukumbi wa Abla Beach Apertment Kibweni Mjini Unguja
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Ali Abdul-gulam akizungumza machache na kumkaribisha mgeni Rasmi Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma kuhutubia na kufungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wanawake wanaomiliki Shule na Vyuo vya elimu ya kati Tanzania (TAWOSCO) uliofanyika Ukumbi wa Abla Beach Apertment Kibweni Mjini Unguja
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akizungumza wakati alipokua akiwahutubia wanafunzi na wanachama wa Umoja wa Wanawake wanaomiliki Shule na Vyuo vya elimu ya kati Tanzania TAWOSCO wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Umoja huo uliofanyika Ukumbi wa Abla Beach Apertment Kibweni Mjini Unguja
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wanaomiliki Shule na Vyuo vya Elimu ya kati Tanzania (TAWOSCO) upande wa Zanzibar Zayna Said Hassan akizungumza wakati alipokua akitoa neno la shukurani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa Umoja huo uliofanyika Ukumbi wa Abla Beach Apertment Kibweni Mjini Unguja,
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akipokea zawadi maalum kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wa Wanawake wanaomiliki Shule na Vyuo vya elimu ya kati Tanzania TAWOSCO uliofanyika Ukumbi wa Abla Beach Apertment Kibweni Mjini Unguja,julai 08,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar
Mke wa Raisi wa Zanzibar Mama Mariyam Mwinyi amewataka wamiliki wa skuli na vyuo vya elimu ya kati kujikita katika kuwapatia stadi za maisha watoto, ambazo zitawasaidia kujilinda na vitendo vya ukatili
Akifungua mkutano mkuu wa jumuiya ya wamiliki wa skuli binafsi na vyuo vya elimu ya kati Tanzania na Zanzibar kwa niaba yake Naibu spika wa baraza la Wawakilishi Mhe Mgeni Hassan Juma, amesema hatua hiyo itapunguza vitendeo hivyo katika jamii.
Amesema kumekua na wimbi kubwa la mmong’oyoko wa maadili ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vitendo hivyo na kuleta athari kwa taifa.
Hata hivyo alisema kuanz.ishwa kwa jumuia hiyo kutasaidia kuimarisha miundombinu Bora ya kusimamia maadili katika jamii na kuwaletea maendeleo
Vilevile aliahidi kuzitatua changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ili kuweza kufkia malengo waliyojiwekea
Nae Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdul-Ghulam Hussein,amesema wizara itahakikisha inashirikiana na taasisi ya Tawosco kuhakikisha wanatatua matatizo yanayo zikabili skuli binafsi ikiwemo Ada elekezi.
Akisoma risala ya taasisi hiyo Mercy Sila,amesema licha ya mafanikio mengi wanayoyapata lakini bado wanakabiliwa na matatizo mbali mbli ikiwemo gharama ya kuendesha skuli, kutozwa kodi nyingi katika skuli zao hali inayopelekea kuzorotesha maendeleo yao.
Mkutano huo ni wapili kufanyika toka kuanzishwa kwa umoja wanawake wanaomiliki Skuli na vyuo vya Elimu ya kati Tanzania TAWASCO ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu ni “Wanawake ni waeelimishaji wa asili na waundaji wa maadili”