Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Ivestment Dkt Fredy Msemwa akizungumza katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu miradi mipya ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Ivestment Dkt Fredy Msemwa akijadiliana jambo na Bw. Raphael Mwabuponde Meneja Masoko na Mauzo wa WHI katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu miradi mipya ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni.
Bw. Raphael Mwabuponde Meneja Masoko na Mauzo wa WHI na Afisa Uhusiano na Masoko Watumishi Housing,Maryjane Makawia wakijadiliana jambo na mmoja wa wateja katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu miradi mipya ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Ivestment Dkt Fredy Msemwa akijadiliana jambo na baadhi ya wateja waliofika katika banda hilo kwenye maonesho ya sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Ivestment Dkt Fredy Msemwa akiwakatika picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo kwenye banda lao.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Shirika la Watumishi Housing Investment (WHI) wanatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa Nyumba za Kisasa katika maeneo ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo tarehe 7/7/2023 Jijini Dar es Salaam Katika Maonesha ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fredy Msemwa, amesema kuwa mradi wa Nyumba za Mikocheni utawasaidia watumishi wa umma kupata nyumba bora kwa gharama nafuu.
Dkt. Msemwa amesema kuwa
wanaendelea na utekeleza ujenzi wa miradi ya nyumba katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Dodoma pamoja kuanza kuuza viwanja katika jiji la Arusha.
“Nawakaribisha wananchi kutembelea banda letu katika maonesho ya sabasaba ili washiriki katika uwekezaji au kupata nyumba katika Mikoa ambayo WHI wana miradi” amesema Dkt. Msemwa.
Dkt. Msemwa ameeleza kuwa watanzania wote, vikundi pamoja taasisi wanapaswa kutembelea katika Banda la Watumishi Housing Investment ili kujionea huduma mbalimbali wanazotoa.
“WHI wapo kwa ajili ya kuwaonesha watanzania huduma na bidhaa ambazo wanatoa kwa wananchi”
Hata hivyo amefafanua kuwa wanaendelea kutambulisha Mfuko wa Faida Fund kwa watanzania ambao umekuwa na mwitiko mkubwa kwani mpaka sasa kuna watu 10,000.
“Mfuko unakuwa kwa kasi na unaonesha manufaa makubwa kwa wawekezaji ambao ni watanzania wa kawaida, taasisi pamoja na Mashirika” amesema Dkt. Msemwa.
Watumishi Housing Investments (WHI) ni taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) iliyoanzishwa mwaka 2014 chini ya sheria ya Makampuni (Cap 212) kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma na wanachama wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Uwekezaji unafanyika kupita Mfuko wa uwekezaji wa pamoja katika milki (WHI Real Estate Investment Trust Fund au WHI-REIT).
Wawekezaji wa awali katika WHI-REIT ni mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), NHC, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).