Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga kuhakikisha anasogeza huduma kwa ukaribu kwa wananchi amechangia kiasi cha shilingi milioni 3 kwa ajili ya kumalizia na kupauwa ujenzi wa mradi wa ofisi ya mtaa wa mail moja A ulipo katika halmashauri ya mji Kibaha.
Koka ameyabainisha hayo wakati wa halfa fupi ya harambee ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kuchangia umaliziaji wa ofisi hiyo na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,chama,wananchi pamoja na wadau wa maendeleo.
Mbunge huyo alibainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kuleta chachu zaidi ya maendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo huduma muhimu za kijamii.
“Kipindi cha nyuma eneo hili kulikuwa na kichaka lakini kutokana na mji wetu unakuwa zaidi ndio maana maendeleo tunayaona kama haya uwepo wa ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa pamoja na kuwepo kwa kituo cha polisi kwa hivyo hii ni moja ya hatua kubwa ndugu zangu,”alisema Koka.
Aidha Mbunge huyo alisema nia yake kubwa ni kuendelea kuleta maendeleo zaidi na kuwataka wana ccm kumpa ushirikiano wa kutosha wakati yupo madarakani na kufanya siasa zenye tija na nidhamu kuliko kufanya mambo ambayo hayana manufaa katika.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa maili moja A Yasin Mudhihir amemshukuru Mbunge Koka kwa juhudi zake za kuungana na wananchi katika harambee hiyo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa ofisi hiyo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza kwa urahisi majukumu ya kuwasikiliza wananchi juu ya changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili.
“Kwa kweli tunamshukuru kwa dhati Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini kwani ameweza kuendelea kushirikiana bega kwa bega wananchi wake na kwamba ameendelea kutuchangia kiasi cha milioni tatu kwa ajili ya kuweza kupauwa ofisi yetu ili iweze kuanza kutumika rasmi,”alisema Mwenyekiti huyo.
Katika hatua nyingine alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo Mbunge huyo alichangia kiasi cha shilingi laki tano kutoka mfuko wa Jimbo ambazo ziliweza kusaidia katika zoezi la kuanza ujenzi huo.
Naye Diwani wa kata ya mail moja Ramadhani Lutambi amebainisha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mtaa wa mail moja kupata urahisi wa kuonana na viongozi.
Kwa kipindi cha muda mrefu mtaa wa maili moja A umekuwa ukikabiliwa na kuwa na ofisi yao ya kudumu kwa ambayo walikuwa wakiitumia katika shughuli zao walikuwa wamepewa kwa muda hivyo ofisi yao ikikamilika itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi na viongozi husika.