WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki,akiwa ndani ya gari mara baada ya kukabidhi Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki,akizungumza wakati akikabidhi Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Lazaro Londo,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia elimu Dkt.Charles Msonde ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki (hayupo pichani),akizungumza wakati akikabidhi Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki,akikata utepe kuashiria kukabidhi Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki,akiwa ndani ya gari mara baada ya kukabidhi Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
Muonekano wa magari yaliyotolewa kwa Maafisa Elimu wa Sekondari kwa Halmashauri 51
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi Magari kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 hafla iliyofanyika leo Julai 5,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Angellah Kairuki amekabidhi magari kwa maafisa elimu sekondari wa Halmashauri 51 huku akitoa rai kwao kutumia magari hayo kama nyenzo muhimu ya kufuatilia na kusimamia utoaji wa elimu bora nchini.
Aidha amewataka wakurugenzi wa halmashauri kusimamia matumizi sahihi ya magari hayo na kutenga bajeti ya matengenezo.
Waziri Kairuki ametoa maelekezo hayo leo Julai 5,2023 Jijini Dodoma wakati akikabidhi magari hayo ambayo ni miongoni mwa magari 200 yaliyonunuliwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 20.6.
“Tunaamini kwamba hakutakuwa na visingizio kwa ninyi kutembelea na kukagua shule pia kashughulikieni kero za walimu huko shuleni kwao badala ya kuwasubiri wawafuate ofisini,”amesema Kairuki
Aidha amewataka Maofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri 51 zilizopata magari mapya kuyatumia vizuri ili kuongeza ufanisi na ubora wa elimu kwenye maeneo yao.
”Nawaomba sana Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia matumizi sahihi ya magari hayo na kutenga bajeti za matengenezo.”amesema
Hata hivyo amewakumbusha kwenda kusimamia kwa karibu ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari unaoendelea nchi nzima.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia elimu Dkt.Charles Msonde amesema magari hayo yanagaiwa kupitia Programu ya LIpa Kulingana na Matokeo katika sekta ya elimu(EP4R) ambapo mpaka sasa tayari magari 146 yameshagaiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Lazaro Londo ,amesema ugawaji wa magari hayo ni sehemu ya utekelezaji es Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ugawaji wa magari hayo ni muendelezo wa juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo katika awamu tatu za awali magari 95 yalipokelewa nak ugaiwa.