Na Ahmed Mahmoud
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kwamba  takribani watu 132 ,000 hapa nchini, wanaambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka huku watu 25,800 wakiripotiwa kufa sawa na wastani wa watu 70  wanaopoteza maisha kila siku Kutokana na TB.
Ameyasema hayo jijini Arusha wakati  akifungua mkutano wa siku tatu wa makatibu wakuu na waratibu wa mipango ya  nchi ya kupambana na  kifua kikuu kutoka nchi 11 za Afrika .
Ummy alisema kuwa, lengo la mkutano huo ni kujadili jinsi gani nchi za Afrika zinaweza kuja  na ubunifu na mikakati  mipya ya kutokomeza  ugonjwa wa kifua kikuu Afrika na duniani kwani takwimu za kidunia zinaonyesha kuwa takribani watu  milioni 10.5  wanaambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka.
Alisema kuwa, kati ya hao takribani watu milioni 1.6 wanafariki kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu kwa mwaka huku serikali ikiendelea mahitaji ya vifaa na matibabu bure sanjari na kufanikiwa kuweza kugundua TB sugu.
“Tulikuwa na mlipuko wa ugonjwa  Uviko 19 na hatukuwahi  kufikia vufo hivi, lakini TB ni kama ugonjwa wa maskini haujapata sauti au mwitikio  kutoka kwa viongozi na jamii namna ya kuutokomeza.”alisema.
Alisema ,serikali kwa kushirikiana na mfuko wa dunia wa kupambana na kifua kikuu ukimwi na malaria (Global Fund) wameweza kukutana ili kuona jinsi gani ya kufikia malengo ya kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030.
“Sisi kama Tanzania tunaona hili  linawezekana mwaka 2015 tulikuwa tunaibua  wagonjwa wa kifua kikuu kwa  asilimia 39 lakini  tuliongeza  jitihada hadi  kufikia asilimia 65 kwa kuwatumia  wahudumu wa afya  ngazi ya jamii.”
Alisema wizara yake ina  mkakati wa kuwekeza kwa jamii sanjari na kutoa mafunzo ya miezi mitatu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 5,000 kila mwaka na kuyatumia  maduka ya dawa baridi na waganga wa tiba asili katika mapambano ya TB hala nchini. 
Awali mkuu wa masuala ya kifua kikuu kwenye mpango wa dunia wa kupambana na TB na Malaria mfuko wa kupambana na dkt. amesema kwamba mfuko huo unasaidia zaidi ya nchi 100 Kote ulimwenguni ikiwemo Tanzania.
Amesema ugonjwa wa kifua kikuu unauwa watu wengi zaidi duniani hasa nchi maskini ambazo zina watu wengi mkutano huu tumeuleta hapa nchini kwani imeonyesha Tanzania ni kinara 
Alisema kwamba shirika lao limekuwa likitoa Takribani dola milion 800 kwa mwaka katika mapambano ya kifua kikuu Malaria pamoja na Ukimwi ambapo Takribani dola bilion 4 kwa bara la Afrika.