Na Lucas Raphael,Tabora
Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora limefanikiwa kuwakamata watumishi wanne wa kampuni ya JV. SPEK LIMITED ya hapa nchini inayojenga mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanzania na kuwafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya wizi mafuta diesel Lita 7,441.94 mali ya kampuni hiyo.
Awali Mwendesha mashtaka wa Polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliwataja majina yao watuhumiwa hao mbele ya hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Igunga Lyidia Ilunda.
Kuwa ni pamoja na Ally Athumani, (36) muongoza mtambo kijiji cha Bulyang’ombe wilaya ya Igunga, Samwel Mtenga(35), mwongoza mtambo kata ya Nanga wilaya ya Igunga. Awaz Mrango (36), muongoza mtambo kata ya Nanga na Zuberi Pastory Ally (41) dereva mkazi wa kijiji cha Bulyang’ombe .
Mwendesha Mashtaka huyo aliiambia Mahakama kuwa Washtakiwa wote wanne wanashitakiwa kwa kosa la wizi wa mafuta ya kampuni hiyo ya JV. SPEK Limited waliyokuwa wakifanyia kazi katika kijiji cha Bulyang’ombe kata ya Nanga wilaya ya Igunga.
Majid aliendelea kuiambia Mahakama kuwa katika tarehe tofauti kati ya 01/05/2023 na 18 /06/2023 huko maeneo ya Kata ya Nanga katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora washtakiwa wate wakiwa waajiliwa wa Kampuni ya JV. SPEK Limited ambayo ni Mkandalasi wa ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta.
Kutoka Uganda hadi Tanzania waliiba lita 7,441.94 mafuta ya diesel yenye thamani ya milioni 20,093,238 mali ya kampuni hiyo ya JV. SPEK Limited na kutumia kwa maslahi yao binafsi na kuisabababishia hasara kubwa kampuni hiyo.
Majid aliambia Mahakama kuwa washtakiwa wote wanne walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 258 (1) 271 kanuni ya Adhabu sura ya 16 mapitio ya 2022 inayozuia kutenda makosa kama hayo.
Hata hivyo baada ya washtakiwa kusomewa shitaka hilo wote kwa pamoja walikana kutenda kosa hilo ambapo mwendesha mashitaka aliiambia Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuahirishwa hadi 31/07/2023 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali na washtakiwa wote wako nje kwa dhamana ya milioni 5,000,000/= kila mmoja kwa .