Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa Klabu Bingwa Tanzania Yanga umewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujiandaa kupokea taarifa za usajili wa kushtua ambao utawafanya waendelea, kutamba katika soka la Afrika.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe amesema kuwa wiki hii, Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo watapokea taarifa nzuri za usajili na mambo mengine ya maendeleo ya klabu hiyo ambayo yataendelea kutikisa.
“Baada ya kumtangaza kocha mpya Miguel Gamondi, hatua inayofuata ni kwenda kwenye uzinduzi wa jezi ambazo tutazivaa kwa msimu ujao wa mashindano na baada ya hapo ni kuanza kutambulisha majembe mapya ambayo yataitumikia Yanga kwa msimu ujao,” alisema Kamwe.
Aliongeza: “Hivi ninavyoongea ‘thank you’ bado hazijaisha tunatembeza kwanza hizo, halafu tunazindua jezi baada ya hapo sasa kazi ya kuleta wachezaji wapya inaanza.”
Alisema kuwa wachezaji watakaosajiliwa si tu kwamba watakuja kuitumikia na kuipa Yanga mataji, lakini pia wataiongezea thamani klabu hiyo ambayo ni Mabingwa wa Tanzania Bara na Kombe la ‘FA.
“Wananchi wajiandae kupokea wachezaji wa mpira kwelikweli ambao viongozi wamewaongeza kwa ajili ya ku- saka mafanikio ya msimu ujaó, kwa hiyo wasiwe na wasiwasi, uongozi wao unafanya kazi kwa weledi mkubwa, wakae wakijua wiki ijayo itakuwa ni ya furaha sana kwao tunakwenda kufanya mambo makubwa sana na nawahakikishia wiki itaanza na moto itamalizika na moto,” amesema Kamwe.
Amesema pia wameingia mikataba na makampuni mbalimbali yatayoidhamini klabu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano yote.
Klabu hiyo itaanza msimu mpya ikiwa na Kocha mpya baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wake, Nasreddine Nabi ambaye hakuongeza mkataba kufuatia ule wa mwanzo kumalizika.
Pia Yanga inatarajia kuanza kambi yake rasmi wiki ijayo tayari kwa ajili ya kujiandaa na msimy mpya wa Ligi Kuu.