WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mheshimiwa Jackson Kiswaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Kaimu mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijimi (RUWASA) Bwai Biseko, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Taifa, Mhandisi Mbogo Futakamba ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Maji wa Taifa hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUWASA Mhandisi Ruth Koya,akitoa neno la shukrani kwa Waziri a Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Maji Mhandisi Abdallah Mkufunzi ,akitoa neno la shukrani kwa Waziri a Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua akizungumza Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji wa Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini hafla iliyofanyika leo Juni 27,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,ameiagiza Bodi ya Mfuko wa Maji wa Taifa kutafuta vyanzo vingine vya Mapato badala ya kuendelea kutegemea fedha zinazotolewa na Serikali.
Waziri ameyasema hayo leo Juni 27,2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za Mfuko wa Maji Taifa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini.
Amesema Mfuko wa Maji ni kichochoe kikubwa cha ukuaji wa Sekta ya Maji hivyo miradi inayotekelezwa isimamiwe ili ikikamilika iwe chanzo Cha mapato na kuwezesha Ujenzi wa Miradi mingine.
“Serikali inatupatia fedha za mfuko wa Maji kila mwezi lakini Bodi hatupaswi kuendelea kutegemea chanzo kimoja kwani mahitaji bado mengi hivyo tutafute namna nyingine ya kupata fedha, mbona kuna taasisi zinapata fedha na sisi tutafute vyanzo vingine vya mapato”amesema Aweso
Aidha, Aweso ameitaka Bodi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kuangalia namna ya miradi ya maji inavyoweza kujiendesha yenyewe katika maeneo ya vijijini.
“Fedha za miradi ya maji zisiachiwe Jumuiya lazima kuwepo na usimamizi lazima sasa tujipime kama kuna haja ya kuendelea na mfumo huu wa kutumia jumuiya kuendesha miradi ya maji vijijini.”amesema
Hata hivyo amesema kuwa hivi sasa wizara hiyo imeshamaliza mchakato wa bajeti yake kazi itakayofuta ni kufanya tathimini ya utendaji kwa watumishi wake na kila mtumishi atawajibishwa.
“Nipo tayari kuonekana mbaya hivi sasa lakini siyo taasisi hii kufia mikoni mwangu ni lazima tufikie malengo ya taifa kwenye upatikanai wa maji mijini na vijijini,fedha zilizotolewa na serikali lazima zitumike kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo ”amesema Aweso
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema kwa sasa Wizara hiyo imeamua kuachana na utaratibu wa kuchimba visima vidogovidogo Kwa Kila Kijiji badala yake wanachimba kisima kikubwa na kusambaza maji katika vijiji vingi ili kupunguza gharama.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema kuwa Dodoma bado hakuna maji ya uhakika hivyo kaiomba Wizara ya Maji kufanya Dodoma kuwa ni eneo Maalum la kushughulikiwa kwani ni Makao Makuu ya nchi hivyo ongezeko la watu wanaohamia ni kubwa.
“Kutokuwepo Kwa maji ya uhakika inaupotezea Mkoa wa Dodoma sifa Kwa wawekezaji maana wanapokuja jambo la kwanza kutuliza ni maji na wakigundua kuwa Kuna changamoto ya maji hawarudi tena hivyo Dodoma kama Makao Makuu itengewe fungu maalumu kuhakikisha changamoto ya maji inatatuliwa ili wawekezaji wavutiwe kuwekeza hapa,” amesema Mhe.Senyamule
Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijimi (RUWASA) Bwai Biseko,amesema kuwa hadi kufikia Desemba 2022, jumla ya miradi 2,273 ya miundombinu ilikuwa imejengwa na kukamilika kupitia fedha za ndani na wadau wa Maendeleo.
“Miradi hiyo inanufaisha wanachi 11,641,230 katika vijiji 4,809. Katika kipindi hicho ujenzi wa mabwawa saba ulikamilika na jumla ya visima 947 vilichimbwa”amesema
Hata hivyo amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2019 hadi September 2022, RUWASA ilifanikiwa kuunda na kusajili CBWSOs 2,524 na zimeweza kuajiri watalaam 5,586 wa fani za ufundi, uhasibu na kada saidizi ili kuwa na uendelevu wa huduma.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi, vilevile, nikushukuru wewe pamoja na uongozi wa wizara ya Maji kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa majukumu ya RUWASA, kiasi cha Sh.995,638,503,970 kati ya Sh. 1,044,588,249,042 zilizotengwa ambayo ni sawa na asilimia 95 ya bajeti ya RUWASA kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2019/2020 hadi mwaka 2021/2022, fedha ambazo zimewezesha kupatikana kwa mafanikio yaliyotajwa hapo juu”amesema
Hata hivyo alisema katika mwaka 2023/2024, RUWASA imepanga kutekeleza jumla ya miradi ya maji vijijini 1,546 ikihusisha miradi ya ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi maji katika maeneo mbalimbali nchini.