WAKAZI wa Kijiji cha Minyinga kilichopo Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi Mkoani Singida,wamempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Miraji Mtaturu kwa kuwa daraja kati yao na serikali la kupeleka maendeleo na kusema mpaka sasa wana Minyinga hawana deni nae.
Akizungumza Juni 25,2023,katika mkutano wa hadhara wa Mbunge Mtaturu katika Kata ya Makiungu uliokuwa na lengo la kutoa mrejesho wa bajeti kwa wananchi na kusikiliza kero zao,Mwenyekiti wa Kijiji hicho Joshua Ikaku amesema Minyinga ya juzi sio sawa na ya leo.
“Minyinga ilikuwa imesahaulika,lakini leo tunajivunia uwepo wa Mtaturu,kuna siku niliwaambia hapa Minyinga hana deni amelipa yote,
“Kwa juhudi zake leo Minyinga tuna shule nzuri,kwa kweli tunafurahia maendeleo ambayo huko nyuma miaka iliyopita hatukuyaona ,ahsante sana mbunge wetu,umelipa deni na chenji imebaki,”amesema Mwenyekiti huyo.