Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ,akiwaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali Kushiriki Mbio za JKT Marathon 2023 zilizoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ,akiwaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali kufanya mazoezi mara baada ya kushiriki Mbio za JKT Marathon 2023 zilizoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete,akizungumza na akiwaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali walioshiriki Mbio za JKT Marathon 2023 zilizoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa hafla za Mbio za JKT Marathon 2023 zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson,akitoa pongezi kwa JKT kwa kuandaa Mbio za JKT Marathon 2023 zilizoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Jacob Mkunda,akielezea jinsi JKT Marathon inavyosaidia kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo nchini wakati wa hafla za Mbio za JKT Marathon 2023 zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akielezea maadhimisho ya miaka 60 ya JKT wakati wa hafla za Mbio za JKT Marathon 2023 zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani),akizungumza mara baada kushiriki Mbio za JKT Marathon 2023 zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete,akikabidhiwa Tuzo maalum na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa mara baada ya kushiriki Mbio za JKT Marathon 2023 zilizoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zilizofanyika leo Juni 25,2023 Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa JKT Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete amewaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali katika Mbio za JKT Marathon zilizofanyika Jijini Dodoma ikiwa ni shamra shamra za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa (JKT ) Maadhimisho yatakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Mbio hizo zilihusisha makundi matatu mbio za Kilomita 5, 10 na 21 zilianzia uwanja wa Jamhuri na kumalizikia katika uwanja huo.
Akizungumza mara baada ya kuongoza mbio hizo zilizofanyika leo Juni 25 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma Dkt. Kikwete amesisitiza kuendelea kuibuliwa kwa wanariadha wengi zaidi ili kuendelea kuitangaza nchi kimaifa kama miaka iliyopita.
“Niwapongeze JKT kwa maandalizi mazuri mliyoyafanya haya yatasaidia kuibua vipaji zaidi na niwaombe wanariadha wakongwe na wanariadha wa sasa wenye umaarufu wasaidie kuhamasisha na kuibua vipaji vingine
Ameongeza kuwa “ Nchi yetu tunapenda sana mpira wa miguu (soka) lakini mchezo huu miaka ya nyuma imeiletea nchi sifa kubwa sana kwahiyo wanariadha maarufu washirikiane na viongozi kuhamasisha mchezo wa riadha” amesema Dkt. Kikwete.
Hata hivyo Dkt. Kikwete ameitaka JKT liendelee kufanya mbio za Marathon mara kwa mara Jijini Dodoma ili Wananchi waweze Kushiriki na kuimarisha afya zao.
Amesema ni wakati kwa JKT mbali na malezi kwa vijana watumike kuibua vipaji mbalimbali kwa vijana hao ili kuweza kulileta sifa nzuri taifa letu kwa sababu nchi inavipaji vingi sana ambavyo bado havijaibuliwa.
“Tanzania lazima tuwekeze kwenye kuibua vipaji ili tuache kutegemea vipaji kutoka nje ya nchi, mfano kwenye mpira wa miguu ligi yetu inasifika lakini wanaoiletea sifa ni wachezaji wanje je wachezaji wetu wa ndani inakuwaje” amesema.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha JKT ili kuweza kuibua vipaji vingi vya wanamichezo hapa nchini ikiwamo riadha.
Amesema JKT imekuwa na timu na wanamichezo mbalimbali wanaofanya vizuri kwenye medani za michezo ikiwamo timu ya wanawake ya JKT Queen na sasa timu mbili za mpira wa miguu JKT Tanzania na timu iliyo chini ya JWTZ ya Mashujaa ya Kigoma.
Ameongeza kuwa “Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kuendelea kuwekeza katika sekta ya michezo ikiwamo kujenga vituo vya kulelea vipaji mbalimbali ambapo vipaji vingi vitaibuliwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM” amesema Mhe. Bashungwa.
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameishauri JKT wakati wakiadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake waangalie namna ya upatikanaji wa vijana hasa wa kujitolea kama utaratibu bado unatija, ili kupitia upatikanaji wa vijana pia utumike kuibua vipaji kwa vijana hao waweze kulisaidia taifa kupitia vipaji hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Jacob Mkunda amesema kupita JKT Marathoni imesaidia kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo, mpaka sasa wameweza kuibua vipaji na kuendeleza vipaji mbalimbali.
”Mpaka sasa tunao wanamichezo wengi ikiwa katika soka tuna timu ya wanawake JKT Queen ambao ni Mabingwa wa ligi Kuu ya Wanawake, JKT Tanzania wanaume na timu ya Mashujaa ya Kigoma wanaamini timu hizo zitafanya vizuri.”amesema Jenerali Mkunda
Awali Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele amesema maadhimisho ya miaka 60 ya JKT imeambatana na shughuli mbalimbali ikiwamo JKT Marathoni ikifuatiwa na maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT itakayofanyika kwenye jingo la SUMA JKT na shughuli nyingine zitatangazwa na JKT shughuli zote zikiwa zimelenga kuitangazia Dunia kuwa JKT inatimiza miaka 60.
Ameongeza kuwa “JKT itaendelea kuhamasisha shughuli za kimichezo hapa nchini ili kusaidia kuibua vipaji mbalimbali vya wanamichezo na kubainisha kuwa maadhimisho hayo yatakuwa ni endelevu ili kuendelea kuibua vipaji” amesema.