Mkuu waWilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA 1984), baada ya kufunga mafunzo yaliyohusu namna bora ya kukuza utendaji katika kuwapa ushauri wanafunzi yalioanza Juni, 21, 2023 na kufikia tamati Juni 23,2023 katika Ukumbi wa TIA Kampasi ya Singida.
…………………………………………..
Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI imewataka washauri wa wanafunzi na viongozi wa serikali za
wanafunzi kuendelea kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na uzalendo, umoja wa kitaifa ili wawe wabunifu ndani ya mazingira ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema hayo Juni 23, 2023 wakati
wa kufunga mafunzo ya washauri wa wanafunzi na viongozi wa serikali za wanafuzi
yaliyoandaliwa na Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa
Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA
1984) ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson.
“Ninyi washauri wa
wanafunzi ndio mtakaoweza kuleta
mabadiliko, nawaomba muendelee kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na uzalendo,
umoja na utaifa, nanyi viongozi wa wanafunzi
shirikianeni vizuri na
washauri wenu ili
msaidie kuokoa maisha ya
wenzenu,’’ alisema.
Apson aliwaomba washauri hao waendelee kuwashauri wanafunzi ili kuunga
mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha wanasoma katika
mazingira mazuri na
kupatiwa misaada stahiki kama
vile mikopo kutoka
Bodi ya Mikopo
HESLB na ZHELB.
Alisema jitihada ziongezwe katika kuwaelekeza kushiriki
kikamilifu katika ukuzaji
na uendelezaji wa vipaji na taaluma kwa lengo la kuimarisha moyo wa
uvumbuzi miongoni mwa
jamii ya vijana
wasomi ili waweze kujitegemea baadaye.
“Waelekezeni kukuza uhusiano
na ushirikiano baina
ya Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Kati, Vyuo vya
Ufundi pamoja na Taasisi za hiari
zinazojishughulisha na masuala
ya elimu, sayansi,
tamaduni na maadili ya
kitanzania, ili kuondokana
na tabia za
kuiga na kujiingiza kwenye
masuala ya ushoga, madawa ya
kulevya na bhangi,” alisema.
Aidha, aliwataka washauri
watumieni na kuwashirikisha wanafunzi kufanya tafiti
zinazohusu changamoto mbalimbali
zinazowakabili ili kupata
usahihi wa yale yanayowasumbua zaidi na hatimaye kuyakabili kwa urahisi.
“Niwashauri muendelee kutumia
mbinu za kisomi
na kisayansi ili
TACOGA1984 ije ijulikane kama
‘Association’ ya wataalamu na wabobevu wa masuala ya ushauri nasaha
(ASSOCIATION OF PROFESSIONAL COUNSELLORS),” alisema.
Mwenyekitiwa TACOGA1984, Bi Sophia Nchimbi, alisema chama hicho kilianzishwa rasmi mwaka 1984 na
kuwa vyuo vilivyoshiriki kwenye mafunzo hayo ni 39 kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar.
Alisema kati ya kazi ambazo wanazifanya ni kutoa ushauri na unasihi katika
ofisi zao na nje wadau wao wakubwa wakiwa ni wanafunzi, wafanyakazi na wengine
kutoka nje ya ofisi zao na pia wanatoa mafunzo ya namna hiyo kwa Serikali za
wanafunzi wa vyuo binafsi na shule za sekondari na kuwafundisha shughuli za mapambano
ya kutokomeza ukatili.
Alitaja kazi nyingine wanazozifanya ni kufanya utafiti na pindi
wanapokutana katika mikutano yao ya kila mwaka huwa wanabadilishana uzoefu
kwani mara nyingi wanapoifanya peke yao inakuwa ngumu.
Alisema mafunzo yaliyotolewa ni kudhibiti migogoro ya wanafunzi katika
vyuo, uongozi wa wanafunzi na usimamizi wa mabadiliko, ukatili wa kijinsia,
kupunguza ukeketaji wa kijinsia vyuoni na kwa wanafunzi kwa ujumla, matatizo ya
afya ya akili, ustawi miongoni mwa wanafunzi, VVU na Ukimwi na masuala
mtambuka, usimamizi wa fedha za wanafunzi, bajeti, utunzaji wa fedha na
ukaguzi, huduma kwa wateja, umuhimu, majukumu changamoto, pamoja na kusimamia
na kuboresha miongozo ya ushauri nasaha.
Alisema pamoja na kazi hizo nzuri wanazozifanya kunachangamoto kadhaa
zikiwemo za ushiriki mdogo wa wadau wao na vyuo kutoka wizara ya elimu, vyuo
vya kati na vyuo vya VETA ambapo wakizungumza nao moja kwa moja wanataka kwanza
wazungumze na wizara husika kwa ajili ya kupata kibali.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, ambapo
yamefanyika mafunzo hayo Dk. James Mrema alishukuru ushirikiano uliopo baina ya
TACOGA na TIA na akaomba udumishwe kwani wote wanajenga nyumba moja hawapaswi
kuwa na utengano.
Dk. Mrema alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya juu kwani imewafanya wanafunzi wengi
kuendelea na masomo ukilinganisha na siku za nyuma.
Mshauri wa Wanafunzi wa Sheria kutoka Chuo cha Sheria Zanzibar, Bi. Sabra
Balyan Suheil akizungumza kwa niaba ya
washiriki wa mafunzo hayo alisema yamewapa mwanga wa vitu vingi ambavyo
walikuwa hawavijui hasa namna ya kumuhudumia mteja ambapo sasa wamepata mbinu
hata za kwenda kuwahudumia waume zao na jamii kwa ujumla.
Mwenyekiti wa TACOGA 1984, Bi. Sophia Nchimbi ambaye pia ni Mshauri wa Wanafunzi (OUT), akitoa taarifa ya chama hicho wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Makamu Mwenyekiti TACOGA 1984, Ndugu Augustine Matemu, akizungumza wakati wakufunga mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Dk.James Mrema (katikati waliokaa), ambaye alimuwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo, Tanzania, Profesa William Pallangyo akizungumza wakati wakufunga mafunzo hayo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa katika ufungaji wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson, akimkabidhi cheti, Naibu Mshauri wa Wanafunzi MUDCC na Katibu Mwenezi wa TACOGA 1984, Bi Zitta Victoria Mnyanyi,
Mshauri wa Wanafunzi wa Sheria kutoka Chuo cha Sheria Zanzibar, Bi. Sabra Balyan Suheil akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo wakati wa ufungaji wa mafunzo.
Mafunzo yakifungwa.
Mafunzo yakifungwa.
Furaha ikitamalaki wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye hafla ya kufunga mafuzo hayo
Mafunzo hayo yakifungwa.
Mafunzo yakifungwa.
Mafunzo ya siku tatu yakifungwa.
Taswira ya ufungaji wa mafunzo hayo.
Mlezi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Mhandisi Saad Hassan ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa TACOGA 1984 (kulia) akiwa na Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha KCMUCo na Mjumbe wa TACOGA 1984, Anza-Amen Lema wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mwangalizi wa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Kampasi ya Singida, Madamu Ambwene Kajula (kushoto) akikabidhiwa chti na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa katika ufungaji wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson.
Mhazini wa TACOGA, Bi. Ruth Kitundu, Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha KCMUCo na Mjumbe wa TACOGA 1984, akikabidhiwa cheti na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.