Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi aliyesimama akiwahutubia viongozi, kulia kwake ni Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Bw Enoch Ngailo na kushoto kwake ni Katibu msaidizi kanda ya kusini Mtwara Bw Philoteus Manula.
Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Mtwara baada ya kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Sekretarieti mkoani Mtwara leo Juni 22,2023.
Na.Mwandishi Wetu.
Viongozi wa Umma mkoani Mtwara wametakiwa kujiepusha na mgongano wa maslahi wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku ili kujenga imani kwa serikali na wananchi wanaowaongoza.
Kauli hiyo, imetolewa na Kamishna wa Maadili Mh Jaji Sivangilwa Mwangesi katika kikao chake na viongozi mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mkoani Mtwara leo Juni 22,2023.
Mh Mwangesi katika hotuba yake amefafanua kuwa, kiongozi wa umma akifanya kazi kwa uadilifu atatoa huduma bora na taratibu, kanuni na sheria na kwamba mianya ya mgongano wa maslahi utapungua.
Mh Mwangesi amebainisha kuwa, kiongozi akiwa muadilifu, atakuwa jasiri katika kutoa maamuzi ya
haki uwazi na usawa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Aisha Mhe, Mwangesi ameongeza kuwa,kiongozi akiwa muadilifu atafata taratibu na sheria pia atasimamia misingi ya maadili ya viongozi kwa uwazi bila upendeleo na kwamba wananchi watakuwa na imani na viongozi wanaowaongoza.
Kuhusu suala la zawadi Mh Mwangesi amewakumbusha viongozi hao kuwa, sheria inamtaka kiongozi kupokea zawadi isiyozidi shilingi laki mbili, iwapo zawadi hiyo itazidi kiasi hicho anatakiwa kuipeleka kwa Afisa masuhuli kwa ajili ya kuitolea maamuzi.
Kamishna wa maadili amefanya kikao hicho na viongozi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma kitaifa iliyoanza rasmi tarehe 16 juni na inatarajiwa kukamilika tar 24 juni 2023.
Kikao hicho cha viongozi wa mkoa wa Mtwara kimehudhuriwa na vionhozi zaidi ya 50 kutoka katika Taasisi za umma na mashirika ya umma pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara.