Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano katika Wizara na taasisi mbili mbali za SMZ na habari maelezo Tanzania bara katika ziara ya kimasomo iliyoanza tarehe 19 -23 June 2023 tarehe 20.06.2023 katika ukumbi wa Mkutano wa ofisi yake Jijini Dodoma.
Baadhi ya maafisa habari mawasiliano na uhusiano wakimsikiliza katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uranium Dkt.Jim Yonazi katika muendelezo wa ziara yao kimasomo katika ukumbi wa Mkutano wa ofisi yake jijini Dodoma.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka Maafisa Habari Mawasiliano na uhusiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa wabunifu katika utekelezaji wa Majukumu yao ya kila siku.
Ameyasema hayo jana wakati alipotembelewa na maafisa hao katika ofisi yake jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza utekelezaji kazi kwa vitengo vya habari na mawasiliano kwa ndugu zao Tanzania Bara.
Dkt.Jim amesema ipo haja ya maafisa habari kubadili mitazamo katika kuhabarisha umma kwa kuangalia mabadiliko ya kiteknolojia kwa kutumia mifumo ya kisiasa inayoendana na wakati uliopo.
“Endeleeni kuwa wabunifu katika kuibua habari na si kusubiri matukio ya viongozi ndipo uhabarishe umma hakikisheni teknolojia haiwaachi nyuma “alisisitiza Dkt.Jim.
Aliwakumbusha maafisa habari katika utekelezaji wa majukumu ya habari ni muhimu kutekeleza sera na mipango ya Serikali.
“Katika utekelezaji lazima tuwe mbele kueleza sera ya nchi yetu na kuelezea miradi mikubwa inayotolewa na nchi yetu”. alisisitiza Dkt. Yonazi.
Aidha aliwahimiza maafisa kujifunza lugha zaidi ya moja ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya kuhabarisha umma ikiwemo kingereza, kifaransa na kichina ili kuwafikia watu wengi na kwa urahisi.
Ziara hiyo ya Maafisa Habari Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika taasisi za Serikali ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania huko Dodoma imeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ikishirikiana na Habari Maelezo Tanzania Bara kwa lengo la kujifunza, ambayo imeanza tarehe 19 – 23 June 2023 Jijini Dodoma.