Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kuratibu
upatikanaji wa madaktari bingwa, vifaa tiba na misaada mingine kutoka kwa
wahisani kwa ajili ya kuboresha sekta ya Afya nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo tarehe 17 Juni 2023 na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na
Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Stephen P. Mbundi wakati wa zoezi la watumishi wa Wizara hiyo kufanya
usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za
kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.
Balozi
Mbundi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo, alisema kuwa
Wizara kwa nafasi yake inaendelea na mkakati wa kutangaza utalii tiba hasa kwa
nchi jirani, na mafanikio yamenza kuonekana kutokana na sekta ya afya nchini
kuimarika na kuwa na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa kwa gharama nafuu
ukilinganisha na maeneo mengine duniani.
Aliendelea
kueleza kuwa watumishi wa Wizara ni sehemu ya jamii ya Watanzania na uamuzi wa
kufanya usafi katika hospitali hiyo ni moja ya jukumu lao la kuhudumia jamii,
kwa sababu usafi ni tiba ya magojwa.
Kwa
upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa Hatarishi, Dkt. Paul Julius Mageni
ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo ameishukuru Wizara kwa
uamuzi wake huo wa kizalendo. Alisema kitendo kilichofanywa na watumishi wa
Wizara ni ibada kubwa na kina lenga kuzuia maambukizi ya magonjwa. “Njia nzuri
na rahisi ya kutibu ugonjwa ni kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na usafi ni moja
ya njia za kuzuia magonjwa kusambaa”, Dkt. Mageni alisema.
Wizara
inaendelea kuadimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili
watumishi ili kuchagiza ari na motisha kwa watumishi kufanya kazi kwa juhudi na
maarifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Kawina Kawina naye akiendelea na zoezi la usafi |
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Athuman Nkungu akiendelea na zoezi la usafi |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi kwa kuchoma takataka |
Zoezi la usafi likiendelea |
Watumishi wa Wizara wakijituma katika zoezi la usafi |
Zoezi la usafi likiendelea |
Zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma likiendelea |
Zoezi la usafi likiendelea |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na zoezi la usafi |
Zoezi la usafi likiendelea |
Zoezi la usafi likiendelea |
Zoezi la usafi likiendelea |
Watumishi wa Wizara wakishiriki zoezi la usafi |
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
|
Balozi Mbundi (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu mara baada ya Wizara kukamilisha zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma |
Picha ya pamoja
|
….Ushiriki wa Wiki ya Utumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara-Dar es Salaam
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam nao wakishiriki zoezi la usafi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023 |
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara waliopo Dar es Salaam wakiendelea na zoezi la usafi katika Taasisi ya Sratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma |
……..Ushiriki wa Wiki ya Utumishi wa Umma katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar wakishiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Rahaleo kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023 |