Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mtembezi Adventure,Samson Samweli akimkabidhi jezi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri kwa ajili ya kukimbia katika mbio za Mtembezi Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya Mbio za Mtembezi ambazo zinatarajia kufanyika Julai 1,2023 Jijini Dodoma zilizoandaliwa na Mtembezi Adventure Kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mtembezi Adventures,Samson Samweli,akielezea lengo la mbio za Marathon kufanyika Dodoma ni kutangaza Utalii na Vivutio katika jiji hilo.
Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Jeshi la uhifadhi Ofisi ya TANAPA Dodoma Dkt.Noelia Myonga,akiipongeza Taasisi ya mtembezi Adventures, kwa kufanya Mbio za Marthon kwa lengo la kuhamasisha Utalii kwa Ubunifu wa hali ya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mtembezi Adventure,Samson Samweli akimkabidhi jezi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri kwa ajili ya kukimbia katika mbio za Mtembezi Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mtembezi Adventure,Samson Samweli akimkabidhi jezi Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Jeshi la uhifadhi Ofisi ya TANAPA Dodoma Dkt.Noelia Myonga kwa ajili ya kukimbia katika mbio za Mtembezi Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,amezindua Vifaa vya Michezo vitakavyotumika katika Mbio za Mtembezi Marathon 2023 zenye lengo la kuhamasisha utalii wa ndani pamoja kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Jijini Dodoma.
Akizingumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua amesema kuwa utambulisho rasmi wa maandalizi ya Mbio za Mtembezi zitakazofanyika Julai 1,2023 Jijini Dodoma ambazo zimeandaliwa na Mtembezi Adventure Kwa kushirikiana na Ofisi yake kwa lengo la kuhamasisha Utalii wa Ndani.
Shekimweri amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuvitangaza vivutio vingi vya kihistoria vilivyopo mkoani hapa huku vingi vikiwa vimebeba historia ya Mkoa wa Dodoma
“Dodoma tuna michoro ya mpango,mapori ya swagaswaga na wanyama wapo,tunataka kupitia mbio hizi za Mtembezi watu wajue Dodoma ni sehemu ya Utalii Kwa kuwa tuna vivutio vya kutosha, watanzania wanatakiwa kuipenda asili yao na kuijua kwa kina hivyo ni wajibu wetu kupitia michezo tuwe vinara wa kutunza asili ya utanzania,”amesema.
Hata hivyo amewataka wadau wa michezo nchini kutumia michezo kutangaza vituo vya Utalii vilivyopo Jijini Dodoma ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutangaza Utalii wa ndani.
“Niwahamasishe watanzania wenzangu kujiandikishe kwa ajili ya mbio hizi tumejipanga kuzifanya kuwa na kiwango kikubwa,kutakuwa na usalama wa hali ya juu na mimi hizi pia ndio kazi zangu,”amesisitiza Shekimweri
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mtembezi Adventures,Bw.Samson Samweli ambao ndio waandaaji wa mbio hizo kwa kushikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma amesema kwa mara ya kwanza mbio hizo zitafanyika mkoani Dodoma Juni mosi mwaka huu ambapo zitakuwa ni za Km 21,10 na 2.5 kwa familia.
Amesema kabla ya mbio hizo kutakuwa na semina kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na vivutio vilivyopo mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Shirika la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA).
“Tumewahi kufanya mbio hizi Bagamoyo, na Tabora Dodoma ndio mara yetu ya kwanza kuja Dodoma, ahadi yetu kwa watanzania ni Mtembezi Adventure kufanya kitu cha kipekee,”amesema Samweli.
Naye Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Jeshi la uhifadhi Ofisi ya TANAPA Dodoma Dkt.Noelia Myonga ,amesema kuwa Tasisi ya mtembezi Adventures, kuwa ni mfano kwa kuwa kinara kuhamasisha Utalii kwa Ubunifu wa hali ya juu.
Amesema,ni muda mrefu sasa kumekuwa na harakati mbalimbali za kuhamasisha utalii lakini Kwa Mkoa wa Dodoma juhudi zaidi Bado zinahitajika na kusema kuwa kupitia mbio hizo itasaidia watanzania kutilia mkazo mambo yote yanayohusu utalii na uhifadhi. .
” Hapa Kikuyu mbali na kuwepo kwa eneo la tembo,ukiingia ndani ya chuo kikuu cha St.Jonh kuna mti mkubwa uliotumika kunyongea wahalifu kipindi Cha utumwa lakini ukiwauliza wanaosoma pale hawajui chochote kuhusu mti huo,”amesema Dkt. Myonga