Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Ilemela wakiwa katika picha ya pamoja na katibu tawala mpya wa wilaya hiyo Wakili Bi Mariam Abubakar Msengi
Katibu wa zamani wa wilaya ya Ilemela Ndugu Said Kitinga akimkabidhi nyaraka katibu tawala mpya wa wilaya hiyo Wakili Bi Mariam Abubakar Mseng
Katibu tawala wa zamani wa wilaya ya Ilemela Ndugu Said Kitinga akifafanua jambo Kwa katibu tawala mpya Wakili Bi Mariam Abubakar Msengi
Katibu tawala mpya wa wilaya ya Ilemela Wakili Bi Mariam Abubakar Msengi amekabidhiwa rasmi ofisi yake leo hii kwaajili ya kuendelea na shughuli za kuwatumikia wananchi
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo, Katibu tawala wilaya ya Ilemela Wakili Bi Mariam Abubakar Msengi mbali na kumshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kumuamini na kumteua kwaajili ya kumsaidia kuwatumikia wananchi wa wilaya ya Ilemela amempongeza kwa utendaji mzuri wa kazi Katibu tawala wa zamani wa wilaya hiyo pamoja na kumpongeza Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Mhe Hasan Elias Masala kwa namna alivyompokea na kumpa ushirikiano
‘.. Nikupongeze kwa utendaji mzuri wa kazi ndio maana Mhe Rais akaona umsaidie katika eneo jingine, Tuendelee kuiendeleza Ilemela yetu ..’ Alisema
Aidha Wakili Bi Msengi ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hasan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na maendeleo
Kwa upande wake Katibu tawala wa zamani wa wilaya hiyo ambae Kwa Sasa amehamishiwa wilaya ya Shinyanga Ndugu Said Kitinga amewashukuru watumishi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilemela kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi pamoja na kuwaomba kuendelea na ushirikiano huo na Kwa Katibu tawala mpya ili aweze kutimiza wajibu wake Kwa ufanisi sambamba na kukemea ukwamishaji Kwa viongozi
Nobert Ndika ni mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilaya ya Ilemela ambapo amewapongeza viongozi wote wawili Kwa kuaminiwa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan pamoja na kuahidi ushirikiano Kwa katibu tawala mpya Kwa niaba ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
Bi Suzana Tumalinywa na Bi Lightness James Kelela ni watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ambao kwa pamoja wamewatakia kheri viongozi hao katika utendaji wao kazi huku wakiwaahidi ushirikiano Kwa kadri ya itakavyohitajika kuhakikisha wananchi wanapata huduma na kutekeleza shughuli za maendeleo
Hafla ya makabidhiano ya ofisi kati ya viongozi hao wawili imeshuhudiwa na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Ilemela katika ofisi za Mkuu wa wilaya hiyo iliyopo Buswelu jijini Mwanza