Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani walipokutana kwa mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake jijini Roma, Italia tarehe 9 Juni, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Roma, Italia. Akishuhudia nyuma yao ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahamoud Thabit Kombo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake jijini Roma, Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake upande wa kulia wakizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani na ujumbe wake walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Roma, Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario walipokutana kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Roma, Italia tarehe 9 Juni, 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario walipokutana kwa mazungumzo jijini Roma, Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu katika picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake (upande wa kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu na ujumbe wake (upande wa kulia) walipokutana jijini Roma, Italia kwa mazungumzo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana na kuzungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani ofisini kwake jijini Rome nchini Italia tarehe 9 Juni,2023
Akizungumza na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Tax ameelezea kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Italia na kuishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo kupitia maeneo ya elimu, afya, kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi wa buluu.
Mhe. Dkt. Tax ameihakikishia Italia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Italia unakuwa na kufikia ngazi ya juu.
Dkt. Tax amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Italia ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo kwa maslahi mapana ya pande zote.
“Nafahamu kuwa nchi zetu hazina mfumo wa majadiliano wa kisiasa na kidiplomasia licha ya kuwa na uhusiano mzuri wa siku nyingi, napendekeza tuanzishe mfumo wa majadiliano ya kisiasa kati ya nchi zetu, mfumo ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizi kwa maslahi ya pande zote,” alisema Dkt. Tax.
Dkt. Tax ameipongeza Serikali ya Italia kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa mpango mkakati wa maendeleo na sera za taifa na kuishukuru kwa mikopo ya masharti nafuu wenye nia ya kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mafunzo ya ufundi na kuwezesha vijana kujiajiri katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza, Songwe, Zanzibar na Dar es Salaam.
Pia ameelezea shukurani za Serikali ya Tanzania kwa Serikali ya Italia kwa mkopo wa masharti nafuu kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao utawezesha utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Taarifa muhimu kwa Tanzania Bara ambapo watoto chini ya miaka MITANO watasajiliwa.
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa Mhe. Anthonio Tajan amesema Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania kama mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kuahidi kuwa Serikali ya Italia itaandaa kongamano la wafanyabiashara ili kuwawezesha wafanyabiashara wa Nchi hizo mbili kufahamiana na kupata fursa za kufanya kazi kwa pamoja.
Amemuhakikishia Mhe Waziri kuwa Serikali ya Italia imedhamiria kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania na nchi za Afrika katika sekta mbalimbali.
Katika tukio jingine Mhe. Dkt. Tax amekutana na kuzungumza na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario jijini Roma na kubadilishana mawazo juu ya njia za kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IFAD ili kuweza kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendeshwa na shirika hilo.
Dkt. Tax pia amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dr. Qu Dongyu. Katika mazungumzo yao Dkt. Tax amepongeza FAO kwa jitihada zake za kutafuta na kukusanya rasilimali kwa ajili ya jamii mbalimbali ili ziweze kunufaika na maendeleo ya kilimo ambazo amesema Watanzania wengi pia wanazitegemea.
Dkt. Tax yuko nchini Italia kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuzungumza na jumuiya ya wafanyabiashara wa nchini Italia.