Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe.Joseph Musukuma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni 9,2023 nyumbani kwake Kilimani jijini Dodoma kuhusu mkataba wa bandari unaotarajiwa kupitishwa na wabunge.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MBUNGE wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe.Joseph Musukuma amekanusha uvumi uliotolewa na baadhi ya watu kuwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepewa fedha ili kuridhia azimio la Bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa mkataba baina ya serikali ya Jamuhri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 9,2023 jijini Dodomaa nyumbani kwake Musukuma amesema wabunge ni wananchi kama wengine na kamwe hawawezi kupitisha kitu ambacho hakina maslahi na Taifa.
“Nataka niwaambie watanzania mimi nilienda dubai tulifanya ziara ya siku 9 kiukweli wao wameendelea kuliko sisi,sasa tumepata hii fursa tunaanza kuponda,tunaanza kutukana hii sio sawa na hao wanaotangaza mitandaoni walishiriki kufanya maovu huko nyuma” Amesema Mhe.Musukuma.
Aidha amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono serikali yao na wabunge kuendelea kuchakata na kupitisha na kama kuna mapungufu yakasimame kwenye mkataba wenyewe.
Mhe.Musukuma amesema ataendelea kupambana na wanaoendelea kuiponda serikali na kusambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii na kuamua kutengeza uongo na kuzua taharuki kwa watanzania na wengine kudai amehongwa ili kutumika kwenye sakata hili la bandari.
”Kutokana na hilo amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kwa wote wanaoeneza taarifa zisizo sahihi ambazo zinalenga kujenga chuki kwa wananchi.”amesema
Hata hivyo amesema kuwa hakuna mradi mkubwa uliotengenezwa hapa Tanzania bila kuwa na makelele,wenzetu dubai wanategemea bandari na airport,tunahitaji kutafuta watu wenye uwezo na kuendesha hivyo.
”Musukuma amesema kuwa mkataba huo hajaona sehemu iliyoandikwa miaka 100 na kama ni miaka 100 ina maana Rais Dkt.Samia Suluh Hassan yuko tayari watanzania wateseke ilihali yeye mwenyewe baada ya kumaliza urais anakuwa mtanzania wakawaida,hivyo amewataka watanzania kuchambua na kuelewa mambo na sio kumezeshwa sumu na baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao hawana maslahi na taifa hili.”amesisitiza
Aidha amesema kuwa anaiomba serikali kama waliweza kuwapeleka wabunge zaidi ya 60 basi waangalie namna ya kuwapeleka waandishi 100 kutoka sehemu tofauti tofauti nchini ili kwenda kushuhudia na kuja kuwa mashahidi kwa watanzania.