Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akipiga marufuku NGOs zinazojishughulisha na ushoga,mapenzi ya jinsia moja na usagaji kuwa hazitakiwa kufanya kazi katika wilaya hiyo.
Aliyesimama kushoto ni Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Lilian Mwelupungwi akimueleza mkuu wa wilaya na afisa tarafa juu ya mikakati ya idara ya maendeleo ya jamii Nchingwea
Na Fredy Mgunda,Nachingwea
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amepiga marufuku kwa taasisi na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kujishughulisha mapenzi ya jinsia moja na ushoga.
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na taarifa na mashirika yasiyo ya serikali, Moyo alisema kuwa hataki kusikia Kuna shirika linapata pesa pahala kwa ajili ya kuhamasisha ushoga na ndoa za jinsia moja kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.
Moyo alisema kuwa ndoa za jinsia moja na ushoga sio utamaduni wa kitanzania na unaharibu nguvu kazi za vijana wengi ambao hugeuka kuwa tegemezi kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.
Alimalizia kwa kuwataka viongozi wa taasisi na mashirika hayo wilaya ya Nachingwea kuwasilisha taarifa zote kwa Mkuu wa wilaya na ofisi ya maendeleo ya jamii ili kutambua kazi zinazofanywa na mashirika hayo.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Lilian Mwelupungwi alisema kuwa taasisi na mashirika hayo kuwasilisha taarifa za wapi wanapata pesa na hizo pesa zinatumika kwa ajili ya nini katika wilaya hiyo.
Mwelupungwi alisema kuwa kuna mashirika na taasisi ambayo hayatoe taarifa kamili juu ya kazi ambazo zinafanywa na shirika husika hivyo kuanzia sasa mashirika yote yanatakiwa kuwasilisha taarifa kila robo ya mwaka katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nachingwea na ofisi ya maendeleo ya jamii.