Vurugu za Chama cha Walimu (CWT) zimeibua sura mpya baada ya baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dodoma Clement Mahemba wamedai kuwa kitendo kilichofanywa na Kamati tendaji cha kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho Japheth Maganga ni uhuni na ukiukwaji mkubwa wa Katiba na Kanuni za CWT.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mahemba amesema kuwa kitendo kilichofanywa na baadhi wa wajumbe wa Kamati tendaji ya chama hicho ni uhuni na kinakiuka Katiba na kanuni za chama.
Amesema taratibu za chama hicho zinaeleza wazi kwenye Katiba ya chama kuwa kama kuna mwanachama anahoja yake zipo njia sahihi za kufuatwa na siyo kama ambavyo wajumbe hao wamefanya.
“Kikao cha kamati tendaji kinazo taratibu rasmi za watu kufikisha malalamiko yao na mwenyekiti ndiye anapaswa kutoa mialiko ya kikao cha kamati tendaji lakini wao wamefanya uhuni wa kuendesha kikao chini ya mti na kuja maadhimio ambayo hanaya msingi mimi niwashauri kama wanajambo lao wasuri vikao rasmi kwani kamati hii haina uwezo wa kumsimaisha katibu isipokuwa baraza kuu ndilo lenye uwezo na baadaye ni mkutano mkuu”amesema
Juzi baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya chama hicho walikutana jijini hapa na kufanya kikao ambacho walikuja na maadhimio ya kumsimamisha katibu wao kujihusisha na shughuli zozote za chama hicho na nafasi hiyo kupewa naibu katibu mkuu.