Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Abdalla Shaibu Kaimu akikagua mradi wa kuku wa kisasa ZAN BREAD LIMITED ambapo aliweka jiwe la msingi mara baada ya kuridhika na maendeleo ya mradi huo huko Mbaleni Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 Abdalla Shaibu Kaimu (mwenye kipaza sauti)akizungumza na wananchi wakati alipotembelea mradi wa kuku wa kisasa ZAN BREAD LIMITED huko mbaleni mkoa wa kaskazini Unguja na kufanikiwa kuweka jiwe la msingi mara baada ya kuridhishwa na mradi huo .
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 Abdalla Shaibu Kaimu akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa kuku wa kisasa ZAN BREAD LIMITED huko mbaleni mkoa wa kaskazini Unguja Juni 3,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Na Rahma Khamis Maelezo
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdallah Shaibu Kaimu amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapiduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi ya kimaendeleo nchini
Pongezi hizo amezitoa huko Mbaleni Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati alipokua akikagua mradi wa ufugaji wa kuku wa kisasa ikiwa ni harakati za mbio za mwenge katika kutembelea miradi mbalimbali Wilayani humo.
Amesema binafsi amefurahishwa na ujenzi wa mradi huo kwani utaongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Aidha amesema Mradi wa ufugaji wa kuku utaleta tija kwa wananchi wa maeneo hayo na vijiji jirani kutokana na kusaidia upatikanaji wa huduma zitakazozalishwa ikiwemo kuku wa nyama. mayai ,uzalishaji wa chakula na mahitaji mengine
Nae Mkuu Mkoa huo Ayoub Muhammed Mahmoud amefahamisha kuwa Serikali imeingia mkataba na Muwekezaji binafsi wa Kampuni ya ZANBREED Limited ili kuleta ajira kwa vijana wa Mkoa huo ambapo ujenzi wa mradi huo umecgharimu milioni saba hadi sasa.
matembezi ya mbio za mwenge wa uhuru 2023 Wilaya ya Kaskazi B miradi mbalimbali ilitembelewa ikiwemo bwawa la umwagiliji maji kisongoni na kupanda miti pembezoni mwa bwawa hilo,pamoja na kutembelea mradi wa tangi la maji Bumbwini amabapo kauli ya mwaka huu kitaifa ni “TUNZA MAZINGIRA,OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA”