RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika eneo lililoandaliwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar, kwa ajili ya uwasilishwaji wa Taarifa za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliyowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Dkt. Othman Abbas Ali, iliyowasilishwa leo 3-6-2023 katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
VIONGOZI mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt.Mwinyi Talib Haji na (kulia kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar.Dkt. Othman Abbas Ali, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG) Charles Kichele na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa, wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar wakati ukipigwa wimbo wa Taifa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar wakati ukipingwa wimbo wa Taifa, kabla ya kuaza kwa hafla ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo 3-6-2023 katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
VIONGOZI wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar Dkt. Othman Abaas Ali, hafla hiyo iliyofanyika leo 3-6-2023 katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.
BAADHI Watendaji Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wageni waalikwa wakifuatilia taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakati ikiwasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Zanzibar Dkt. Othman Abbas Ali.(hayupo pichani) hafla hiyo iliyofanyika leo 3-6-2023 katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.