WANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi cha Meru National Political cha Kenya wamemaliza mafunzo ya mabadilisho katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na kuweza kutunukiwa vyeti mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Wanafunzi hao ambao walikuwa 30 pia wameweza kufanya ziara kutembelea miradi mbalimbali nchini ikiwemo daraja na Tanzanite na kuweza kujifunza mambo mengi kupitiamiradi ambayo inatekelezwa nchini.
Akizungumza katika tukio la ugawaji wa vyeti, Mkuu wa kitengo cha Udahili kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT, Bi Dkt.Triphonia Ngailo ameiomba Serikali iangalie namna ya kuwafadhili wanafunzi wanaosoma ngazi ya cheti na Stashahada katika nyanja ya Sayansi na teknolojia ili kupata wabobezi wa uhandisi ambao watakuwa msaada wa taifa hapo baadae.
Amesema ili kupata wahandisi wazuri na wanaoajirika na kuendana na Sera ya Teknolojia ya Viwanda Serikali inapaswa kuwekeza katika sekta hiyo ya elimu kwa wahandisi.
Kwa upande wake Mkuu wa Usimamizi wa kijamii DIT Dkt.Yasinta Manyele,amesema programu ya kubadilishana wanafunzi wa nchi na nchi inasaidia kuongeza zaidi urahisi wa ajira na kuondoa malalamiko ya ajira.