YANGA SC imejiweka katika mazingira magumu ya kutwaa Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na USM Alger mchezo wa kwanza wa Fainali ya Michuano hiyo uliochezwa dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
USM walipata bao la ushindi dakika ya 32 likifungwa na Aimen Mahious bao lililowapeleka wageni mapumziko wakiwa mbele ya bao hilo.
Mshambuliaji hatari kwa Sasa ndani na nje Fiston Mayele alifunga bao dakika ya 82 likiwa bao lake bao lake la saba katika michuano hiyo dakika ya 84 wageni walipata bao la pili likifungwa na Khaled Bousseliou dakika mbili tu baada ya bao la Mayele.
Kwa matokeo hayo Yanga wanatakuwa kwenda kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili na kuendelea ili waweze kutwa ubingwa wa michuano hiyo mchezo wa marudiano utapigwa Juni 3,mwaka huu nchini Algeria.