Baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah,akitoa elimu kwa wabunge kuhusu mikakati ya Shirika hilo wakati wa kikao cha kuwajengea uelewa wabunge hao kuhusu taarifa ya utekelezaji wa sera ya ubia.
Baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah akielezea mikakati ya Shirika hilo wakati wa kikao cha kuwajengea uelewa wabunge hao kuhusu taarifa ya utekelezaji wa sera ya ubia.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Geoffrey Pinda akiwa katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Lucy Kabyemela.
Baadhi ya maafisa wa NHC na Wizara ya Ardhi.
Mkurugenzi Mkuu, Abdallah akifafanua mambo muhimu kuhusu miradi yao mbalim bali.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii imelitaka
Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) kuzingatia maslahi mapana ya Taifa na
ya Mashirika inapoanza kutekeleza miradi ya ubia ili iwe na tija.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Timotheo Paul Mzava ambaye pia ni Mbunge wa
Korogwe Vijijini amesema kuwa Kamati hiyo inalielekeza Shirika hilo la
Nyumba la Taifa lenye dhamana ya kuendeleza na kusimamia sekta ya
nyumba nchini kufanya upembuzi yakinifu kabla ya hata kusaini mikataba
ya ubia ili miradi hiyo hatimaye iwe na tija na ufanisi kwa Taifa.
“Ni kweli kuwa Serikali ina jukumu la kusimamia sera na mipango ya
nchi na hata kutekeleza na kuongoza sekta ya nyumba, lakini pia ni
kweli kwamba ukweli ni kwamba katika zama za leo huwezi kutegemea
Serikali au taasisi za pekee katika kuwapatia Watanzania Makazi hivyo
ni lazima kushirikisha sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na
makampuni katika kuwapatia wananchi makazi maeneo ya biashara na
Ofisi,”amesema.
Kamati imelipongeza Shirika kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu
yaliyokuwapo katika sera ya ubia iliyopita na imelitaka Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea kufanya kazi kwa mashirikiano na
baadhi ya taasisi, makampuni.
“Msisitizo wetu kama Kamati tushirikishe Sekta binafsi kwani Sekta
binafsi sio tatizo kilichokuwa kikitusumbua ni ile mikataba tuliyokuwa
nayo awali kutozingatia maslahi ya Taifa. Sasa katika sera hii mpya
pamoja na kujieleza vizuri bado msisitizo wetu mashirika na makampuni
endeleni kupigania maslahi ya Taifa na mashirika yenu katika mikataba
hiyo tunayokwenda kuingia na hao wabia,” amesema Mnzava.
Nao wabunge wa Kamati hiyo waliokuwepo katika mkutano huo waliomba
Shirika la Nyumba la Taifa kuangalia maeneo ya kuwekeza huku wengine
wakidai miradi hiyo ya NHC kufika katika mikoa yote ya Tanzania bara
ili watumishi waweze kupata makazi ikiwa na punguzo la gharama.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Taifa, Hamad
Abdallah ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na
Utalii kuwa itahakikisha mikataba ya Ubia itayaoingia na watu ama
Makampuni mbalimbali itakuwa bora zaidi.
Amesema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa katika mikataba itakayoingia
ya Ubia imehakikisha imewachambua wawekezaji kwa kuwatahamini kwa kina
na kuangalia mapendekezo yao na kuwachuja kwa uwezo wao.
“Kupitia Sera yetu hii tumehakikisha tumepitia na uhakiki kwa umakini
taarifa za wabia wetu kwani pamoja na mambo mengine tumezingatia eneo
ambalo mbia anataka kuwekeza ana uwezo nalo na kile ambacho anataka
kuwekeza kitaendelea kuliletea faida Shirika kwa siku za usoni,”
alisema Abdallah
Amesema kikao hicho kimekuja baada ya Kamati kufanya ziara miezi
miwili iliyopita katika eneo la Mradi wa kimkakati wa Tanzanite
Mererani ambapo Kamati ilitaka kujua sera mpya ya ubia iliyozinduliwa
mwaka jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim
Majaliwa Majaliwa. .
Amesema baada ya wasilisho Kamati imefurahia sera mpya ya buia kwani
wameona ni jinsi gani sera hiyo inaweza kuleta tija katika Shirika na
huku wakifarijika kuona yale mapungufu ya awali yaliokuwepo kwenye
sera ya Ubia ya awali yamefanyiwa kazi na kubadilishwa na kuwepo kwa
maboresho makubwa katika sera mpya ya Ubia.
Aidha amesema Kamati hiyo imetoa angalizo kwa Shirika la Nyumba
Tanzania (NHC) kuwa makini wanapopata hao wabia katika kutayarisha na
kusaini mikataba hiyo ili mikataba hiyo iwe na tija katika Serikali.
” Sisi Kama Shirika la Nyumba tumelifanya na kuzingatia na ndio maana
mnaona hatua mbalimballi za utekekezaji, hata pale tunapotangaza mradi
tunakuwa na wasilisho la hao wanaotaka hiyo Miradi na baada ya
wasilisho tunafanya uhakiki na baadaye tunakaa na hao Wabia kwa ajili
ya kujadili masuala mbalimbali yaliyopo kwenye mkataba,” amesema
Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo amesema katika utayarishwaji wa mikataba hiyo wao kama
taasisi ya Serikali wanakuwa na maoni na uongozi wa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali na hatua ya kwanza ya mikataba hiyo tayari imeshapitiwa na
Mwanasheria huyo na baada ya kupitiwa na mwanasheria huyo na
ikarudishwa katika Shirika.
“Katika kila mkataba inakuwa na mambo tofauti tofauti thamani ya Mradi
michoro yake wakishamaliza wabia hivyo sasa wabia wanakwenda
kutayarisha michoro ambayo itaonyesha thamani ya miradi hiyo na
itarudi tena kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali lengo likiwa ni kuwa
makini,” amesema .
Amebainisha kuwa uhitaji wa nyumba Tanzania ni mkubwa sana na NHC peke
yake haiwezi kulimaliza tatizo hilo ndiyo maana inakaribisha
wawekezaji ili kuweza kuungana kwa pamoja kuisaidia Serikali katika
kulitatua tatizo la uhitaji wa nyumba nchini.
Aliongeza kusema kuwa wadau wamekaribishwa kujenga kwenye ardhi yenye
thamani ya shilingi bilioni 72 wakati uwekezaji tarajiwa utakaofanywa
utafikia kiasi cha shilingi bilioni mia tatu arobaini (340).
Akijibu baadhi ya wabunge Mkurugenzi amesema kuwa kuna maeneo ambayo
NHC ilishaanza kuyajenga kwa lengo la kuwaonesha Watanzania makazi
bora yanakuwaje na hiyo haikuzingatia uhitaji wa soko na akaongeza
kusema kuwa hata Baba wa Taifa aliwahi kutekeleza haya.
Moja ya swali lililoulizwa Mhe. Innocent Bilakatwe Mbunge wa Kyerwa ni
kuhusiana na nyumba za makazi Iyumbu Bw. Abdallah alisema kuwa mpaka
sasa jumla ya nyumba mia moja sabini na sita (176) zimeshauzwa na
kwamba zilizosalia mia na ishirini na nne (124) ziko katika mazungumzo
na Taasisi moja ya Serikali imeonesha nia ya kuzichukua zote.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godfrey
Mizengo Pinda amesema Kama Serikali wamejipanga kwasasabu katika
mikataba iliyotangulia inawafundisha kuwa na mikataba iliyo bora bora
na wanakwenda kuboresha .
“Tumekuwa wakiingia mikataba na watu mbalimbali na wenye tabia tofauti
tofauti katika utendaji kazi wao, wengine wamekuwa wakitaka kunufaika
wao kabla ya Serikali, lakini kwa maana ya uanisho mambo
yatakayokwenda kuingia kwenye mikataba ni kulinda maslahi ya Serikali
kwanza na mashirika yaliopo chini ya Serikali.