Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma .
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ,akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma .
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Petro Ngata,akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya washauri wa SUMA JKT Meja Jenerali Mstaafu Farah Mohamed,akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyoni,akitoa taarifa wakati wa hafla ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyoni,wakati wa hafla ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma .
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma .
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akiwa ndani ya gari mara baada ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma .
Muonekano wa Mitambo ya kuzalisha zege na magari yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayotumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) katika eneo la Kisasa leo Mei 23,2023 jijini Dodoma .
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele,amezindua rasmi mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege itakayokuwa ikitumiwa na kampuni ya ujenzi ya Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.349 za kitanzania.
Akizungumza leo Mei 23,2023 katika eneo la Kisasa jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mitambo hiyo Meja Jenerali Mabele,amesema kuwa hatua hiyo ni kubwa wakati JKT ikielekea kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake..
Amesema uzinduzi wa mtambo huo na magari unakwenda kuiwezesha SUMA JKT, kuondokana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kununua zege, kukodi magari na kuzisafirisha kwenye miradi yake mbalimbali, pia itawaingizia fedha kutokana na kuuza zege kwa wakandarasi wengine hapa nchini.
“Tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuiamini SUMAJKT kwa kuipa miradi mingi na ndio maana wanapambana kuhakikisha wanapata mitambo ili kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na tutaendelea kuilinda imani hiyo” amesema Meja Jenerali Mabele
Aidha amewaagiza watendaji wa SUMA JKT kuhakikisha wanasimamia mitambo hiyo ili ilete tija iliyokusudiwa katika kuongeza ufanisi wa SUMAJKT.
“Kwa watakao pewa dhamana ya kusimamia mitambo hiyo lazima wazingatie matengenezo kwa wakati ili mitambo hiyo idumu kwa muda mrefu sio ukiona mtambo unafanya kazi unaendelea kuutumia hali ukijua muda wa matengenezo umefika” amesema
Hata hivyo amesema kuwa JKT inakwenda kuadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwake na sasa ni wakati wa teknolojia ni lazima tuonyeshe mabadiliko kwa kuwa na vifaa vya kisasa katika kutekeleza majukumu.
“Kama mnavyojua SUMA JKT ilianza kama kitengo cha ukarabati lakini kilikuwa na sasa ni shirika kubwa sana hapa nchini na linaloaminika na linalopata miradi mikubwa lazima tuonyeshe utofauti.
Mwanzo tulikuwa tunaingiza vijana wengi mashambani lakini kwa sasa tumeweka mitambo mikubwa ya kiteknolojia mashambani na tunalima kwa tija kubwa kutokana na mitambo tuliyonayo” amesema.
Kwa upande Wake Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Petro Ngata, amesema ununuzi wa mtambo huo ni moja ya mipango ya Shirika hilo ni kununua mitambo ya kisasa katika mwaka wa Fedha 2022/23 huku akiwataka watendaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija.
”Mitambo hiyo itasaidia katika kutekeleza miradi wanayopata na wamejiwekea malengo ya kuongeza vitendea kazi kwa kampuni tanzu za SUMAJKT kuziwezesha kampuni hizo ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.” Kanali Ngata
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya washauri wa SUMA JKT Meja Jenerali Mstaafu Farah Mohamed ameipongeza SUMA JKT kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kutekeleza yote wanayokubaliana katika vikao vya bodi na Shirika hilo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyoni,amesema mitambo hiyo imeingizwa nchini Januari 16, 2023 na kumaliza kusimikwa May 22, 2023 jijini Dodoma, na inauwezo wa kuzalisha zege cubic meter 60 kwa saa, magari matatu yenye uwezo wa kubeba zege cubic meter 8 kila moja na pampu ya kusukuma zege.
”Mtambo na magari hayo yamegharimu Sh.bilioni 1.349 na utawawezesha kuzalisha Zege na kuuza kwenye makampuni mengine.”amesema Mhandisi Nyoni