Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kaspar Mmuya, wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Jijini Nairobi, Nchini Kenya, leo Mei Jumatatu 22, 2023, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA utakaojadili masuala ikiwemo Vitambulisho vya Taifa. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya, Isaac Isanzu.
Na Mwandishi Wetu, MoHA, Nairobi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Kaspar Mmuya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ismail Rumatila wamewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), jijini Nairobi Saa 5:10 asubuhi wakitokea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa ID4AFRICA.
Masauni ataiwakilisha Tanzania katika Mkutano huo utakaojadili masuala mbalimbali ikiwemo katika kuendeleza Ikolojia ya Utambulisho (Identity Ecosystem) kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kidigitali katika maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi kwa binadamu.
Mkutano huo unatarajiwa kuanza Mei 23, 2023 na kumalizika Mei 25, 2023 ambapo utatoa nafasi kwa viongozi wa mataifa mbalimbali kutoa taarifa zao kuhusiana na mifumo hiyo.