MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imedhamiria kuchukua makombe yote manne msimu huu baada ya kuichapa bao 1-0 Singida Big Stars na kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Liti Mjini Singida.
Yanga Sc mpaka sasa imeshachukua Makombe mawili walianza na Ngao ya Jamii,Kombe la Ligi Kuu ya NBC na sasa wapo katika Fainali mbili Kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) .
Yanga SC walianza mchezo kwa kubadilisha kikosi cha kwanza kwa kuwapumzisha nyota wake kujiandaa na Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baadhi ya wachezaji walioanza ni Mauya, Doumbia, Mzize na mlinda lango Metacha Mnata.
Katika mchezo huo ambayo ilikuwa ya aina yake, timu zote zilitengeneza nafasi za magoli kipindi cha kwanza bila mafanikio, hivyo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 0-0.
Kama kawaida kipindi cha pili Prof,Nabi alifanya mabadiliko ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza aliweza kuwaingiza Fiston Mayele, Kennedy Musonda ,Tuisila Kisinda na Dikson Job mabadiliko hayo yalibadilisha mchezo na Yanga kuendelea kuishambulia Singida Big Stars.
Kuingia kwa wachezaji hao kuliipa Yanga SC faida na kuweza kupata bao dakika ya 82 likifungwa na Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele baada ya shuti la Dennis Nkane kupanguliwa na golikipa Benjamin Haule.
Kwa matokeo hayo Yanga Sc imetinga Fainali na sasa itaenda kukutana na Azam FC ambao walitinga hatua hiyo mara baada ya kuwaondoa Simba Sc Fainali hiyo itachezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga Juni Mwaka huu.