SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akipokea zawadi kutoka kwa Viongozi wa Shirika la Posta mara baada ya kutembelea banda la shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma .
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mabanda mbalimbali katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma .
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),Elia Madulesi,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Shirika hilo wakati wa Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma .
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akipokea zawadi kutoka kwa Viongozi wa Shirika la Posta mara baada ya kutembelea banda la shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma .
Na.Alex Sonna-DODOMA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson amelipongeza Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa kuendelea kufanya vizuri katika utendaji kazi wake kwa kufikisha huduma haraka kwa wateja wao.
Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea banda la Shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea viwanja vya Bunge Jijini Dodoma yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Dk.Tulia amesema kuwa amefurahishwa na zoezi la anwani za makazi ambalo lilianzia mapema mwaka jana na kwa sasa wamefikia sehemu ambayo kwa yule aliyesajiliwa namba yake anaweza kuipata kiganjani kwa kutumia aina yoyote ya simu
“Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na Wizara hii ya habari mtu kujua anwani yake ya makazi ni jambo la msingi sana.,”ameeleza.
“Shirika letu la Posta sasa nafikiri mjipambanue zaidi Kwa sababu mmewezeshwa Kwa kiasi kikubwa na zoezi la anuani ya makazi ukimutumia mtu barua inaenda hadi nyumbani kwake kwakuwa tayari namba ya nyumba yake inafahamika hivyo ongezeni nguvu”amesema
Hata hivyo amewataka wananchi ambao hawajasajili makazi yao kusajili Kwani mtu kujua anuani yake ya makazi zinasaidia kupata huduma Kwa haraka na kuchochea maendeleo
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),Elia Madulesi, amesema kuwa Kwa sasa mwananchi anafikiwa Kwa urahisi na huduma za Shirika la Posta Tanzania kutokana na kukamilika Kwa Mradi wa Anuani za makazi ambayo Kwa sasa huduma ya vifurushi,vipeto na barua bila kupotezewa Muda.
“Siyo hivyo tu Kwa sasa Mteja wa POSTA anaona kabisa mzigo wake Jinsia unavyosafirishwa Kwa kutumia mtandao hivyo tumekuwa kidijitali zaidi na baada ya hapo mzigo utamfikia mlengwa Kwa wakati kwani Anuani za makazi zimerahisisha Kila kitu,”
Na kuongeza kuwa “Shirika la Posta na Anuani za Makazi ni mapecha Kwa sababu tangu kuimarishwa Kwa mfumo huu wa Anuani za Makazi mambo yamekuwa rahisi sana na huduma imekuwa na ufanisi,”amesema Madulesi
Madulesi,amesema tangu Anuani za Makazi kukamilike Shirika la Posta limeongeza usambazaja wa vipeto,barua na vifurushi Kwa asilimia 14.
Maonesho ya wadau wa Mawasiliano yanaendelea kwa siku 3 katika viwanja vya bunge ikiwa ni kuelekea kwenye bunge la bajeti ya Mawasiliano iliyosomwa leo na Waziri wa Habari na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Mnauye.