Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) Dr Lin Bin alipowasili Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo jijini Dar es salaam.
Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) Dr Lin Bin (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (kulia) wakiwatazama washereheshaji wa ngoma za asili alipowasili Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo jijini Dar es salaam.
Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) Dr Lin Bin akisaini Daftari la Mahudhurio alipowasili Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni leo jijini Dar es salaam.
Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) Dr Lin Bin akionyeshwa na kuelezewa historia mbalimbali zilizopo katika Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni alipotembelea Makumbusho hiyo siku ya leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akimkabidhi zawadi Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) Dr Lin Bin wakati wakiagana baada ya kutembelea Makumbusho hiyo siku ya leo jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja ya Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) Dr Lin Bin Maafisa na viongozi wa Makumbusho ya Taifa.(picha na Mussa Khalid)
……………………….
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa ujio wa Rais wa chama cha Urafiki cha China na Afrika Dr Lin Bin na Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni utaendelea kukuza ushirikiano katika nyanja za ubalii baina ya mataifa hayo.
Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam baada ya Dr Lin ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa Kamati ya 13 ya Kitaifa ya Mashauriano ya Kisiasa ya Watu wa China (CPPCC) kutembelea Makumbusho ya Taifa na kujionea historia ya Tanzania ambayo imehifadhiwa katika makumbusho hiyo.
Akizungumzia Ugeni huo Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema kuwa utalii wa Makumbusho na Malikale unazidi kukua katika nyanja za kitaifa na Kimataifa kwani ujio wake utasaidia kuendelea kuvutia watalii wengi kutembelea vivutio mbalimbali nchini.
‘Ugeni wake umehamasisha wageni wa kichina kufika Tanzania kupitia makumbusho ya Taifa kwani amejionea vivutio vingi kati yetu na China ameshuhudia uwepo wa viasharia vya urafiki na biashara ya muda mrefu vikiwemo vibakuli vya kichina ambavyo vilitumiwa katika maeneo ya kale ya swahili katika uwanda wa pwani ya Afrika ya Mashariki’amesema Dkt Lwoga
Pia Mkurugenzi huyo amesema Dr Lin ameshuhudia onyesho la Zamadamu wa Kale kwa kuyatizama malikale halisi ya Zinanthropus ambaye aliishi miaka Mill 1.7 iliyopita.
Aidha Dkt Lwoga amesema mgeni huyo ameweza kufurahia onyesho la sanaa za sasa na za miambani ambazo zinaashiria utamaduni wa binadamu wa sasa na wa kale hivyo maeneo hayo ameonyesha nia katika kuonyeza mashirikiano hasa katika nyanja ya utafiti.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni Adelaide Sallema amesema watatumia fursa hiyo katika kufanya tafiti mbalimbali ili kuendelea kuvibaini vitu vingi vyenye uhusiano kati ya China na Tanzania .
Amesema wataendeleza mashirikiano na Taifa hilo ili kuonyesha mafanikio zaidi sekta ya utalii na hivyo kuwavutia wageni wengi kwenda kutembelea vivutio mbalimbali nchini.