WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Prof.Kitila Mkumbo,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Bi. Mtumwa Idd Hamad,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba,akichangia mada wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Buyungu Aloyce Kamamba,akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi.Rose Maliki,akichangia wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiwa na viongozi mbalimbali wakifatilia mada wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu na kumalizika leo Mei 14, 2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akichangia mada wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu na kumalizika leo Mei 14, 2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiteta jambo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu na kumalizika leo Mei 14, 2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael wakati wa Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga Kongamano la kujadili Sera na Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, sekondari na Ualimu lililofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,amesema kazi ya kukusanya maoni ya kuboresha mitaala na sera ya elimu inaendelea, watachakata maoni yote ili kupata kitu kizuri chenye tija kwa taifa.
Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Mei 14, 2023 Jijini Dodoma wakati wa kufunga Kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu lililofanyika siku tatu.
Amesema kuwa nia ya Serikali ni kufanya maboresho makubwa kwenye sekta ya elimu hivyo kamati haitaacha maoni yoyote ambayo yanatija katika kuboresha mfumo wetu wa elimu nchini.
“Niwahakikishie hakuna maoni yatakayoachwa yote tutazingatia na tutayabeba kwa ajili ya utekelezaji nashukuru kuna baadhi ya maoni yametolewa ufafanuzi hapahapa”amesema Prof.Mkenda
Aidha amesema Wizara itazingatia maoni yaliyotolewa na wadau kwenye kongamano hilo na malengo yaliyopo ukusanyaji maoni utaendelea hadi Mei 31, 2023.
“Tumejiwekea malengo ifikapo Mei 31, tuwe tayari kusonga mbele, tulikuwa tunasikiliza kwa makini sana maoni nimeona hakuna upinzani katika mambo muhimu ya mageuzi ya sera.”
“Kuna maoni elimu ya awali iwe ya lazima ni suala ambalo hata kamati ya bunge walisisitiza na sisi tumesema tunalipokea tunalichakata na kuliangalia, hatuwezi kusema kwa haraka kwamba litakuwa lazima lazima tuangalie uwezekano wa utekelezaji,”amesema Prof.Mkenda
Hata hivyo amesema baadhi wameshauri elimu ya lazima iwe miaka 11 ambayo inajumuisha elimu ya awali nayo iwe lazima na sera ya mwaka 2014 ilikuwa inataka elimu ya lazima iwe miaka 10 lakini utekelezaji ulikuwa miaka 7 na kubainisha kuwa watalichakata jambo hilo kwa umakini mkubwa.
Waziri Mkenda amesema kwenye mapitio ya sera yamegusa hadi vyuo vikuu na suala la mitaala litaendelea kuwa endelevu.
“NACTVET wanakamilisha utafiti waliofanya kwa waliohitimu vyuo vya ufundi vya VETA wapo wapi na wanafanya nini, na kuchunguza kwenye magereji, hoteli wameajiri wangapi kutoka VETA.”
Ameongeza kuwa “tunataka tutengeneze elimu ya kiujitegemea na tutengeneze uwepo wa wahitimu wenye uelewa na wenye jeuri ya kuhoji na katika bajeti tumetenga tayari kuwaandaa walimu kuendana na mabadiliko hayo tija ipatikane” amesema.
Hata hivyo amesema kuwa watahakikishie katika mafunzo ya amali hasa tunataka tusiyafanye watu wakayadharau na ndio maana hasa ya kuanza na vyuo vya ufundi, mafunzo ya amali sio ya waliofeli bali waliofaulu vizuri.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Deogratius Ndejembi,amesema kama TAMISEMI haitakuwa kikwazo katika kutekeleza sera mpya ya elimu itakayopitishwa.
Ameongeza kuwa “mpaka sasa tuna shule 9 za ufundi na kupitia mradi wa SEQUIP tuna kiasi cha bilioni 300 tuna kwenda kujenga shule za ufundi katika karibu Halmashauri zote ambazo hazikufikiwa na vyuo vya VETA tunakwenda kujenga madarasa hayo” amesema Mhe. Ndejembi.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Prof.Kitila Mkumbo,amesema wao kama wawakilishi wa wananchi Bungeni watahakikisha wanasimamia maoni yote ya wadau yanafanyiwa kazi kikamilifu ili tija ya kuanzisha zoezi hilo ifanikiwe na baada ya miaka mitano tija ianze kupatikana.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Bi. Mtumwa Idd Hamad amewashukuru viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanziabar kwa miongozo wanayowapa ambayo inarahisisha utendaji kazi wao.
Amesema mabadiliko yanayofanywa yataleta tija kubwa kuhakikisha vijana wanaozalishwa wanakuwa na uelewa wa kutosha na wanaoajirika na wenye uwezo wa kujiajiri wenyewe kutokana na ujuzi wanaoupata.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Dk Angelina Mabula amesema kuwa Wizara yake itawapa ushirikianao wapi mnataka viwanja kwa ajili ya vyuo vya ufundi sisi tutawapatia watanzania tuko mikononi salama kwenye mikono ya Rais Suluhu Hassan na maono yake yatatimia.
Awali,Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,amesema michango iliyotolewa na wadau itazingatiwa kwenye uchakataji ili kuwa na sera na mitaala bora.