Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu Tanzania (TPHPA) Profesa Joseph Ndunguru akizungumza jijini Arusha kuhusiana na maadhimisho hayo.
Julieth Laizer ,Arusha.
Arusha .Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu (TPHPA) ,Dokta Ndunguru amewataka wananchi kutunza mazao yao kwa kufuata kanuni na mbinu za kudhibiti afya ya mimea ili kuweza kuongeza tija na kuchochea ajira na kupunguza umaskini .
Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza katika maadhimisho ya Afya ya mimea duniani yaliyoadhimishwa katika makao makuu ya TPHPA yaliyopo Ngaramtoni mkoani Arusha.
Dokta Ndunguru amesema kuwa,kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kujiwekea dhana ya kutunza mazao yao kwa kufuata kanuni ili yaweze kuongeza kipato kwao na kupata mazao ya kutosha .
Dokta Ndunguru amesema kuwa, asilimia 80 ya chakula cha binadamu kinatoka kwenye mimea ambapo mimea yenyewe imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya visumbufu ,mabadiliko ya tabi ya nchi,na uchomaji wa misitu.
Amesema kuwa,kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Afya ya mimea kwa ajili ya kupunguza umaskini njaa na kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa nchi zetu “.
Aidha amesema kuwa,lengo kubwa la mamlaka hiyo ni kuwa na mfumo mmoja wa kudhibiti afya ya mimea na hatimaye kuweza kuondokana na changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa afya ya mimea katika mamlaka hiyo, Dokta Benignus Ngowi amesema kuwa,wamekuwa wakihakikisha bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kwenda nje ya nchi hazina visumbufu vya mimea .
Ngowi amesema kuwa,wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mimea ,mazao, na vipando vyote kwa lengo la kulinda mimea isivamiwe na wadudu wasumbufu ambapo wana vituo 36 mipakani .
“Huwa tumekuwa tukifanya ukaguzi maalumu katika maeneo ya mipakani kwani huwezi kutambua visumbufu kwa macho ni lazima ufanye ukaguzi wa kutosha ili kujiridhisha na kuweza kuondokana na changamoto mbalimbali.”amesema Ngowi.
Kwa upande wake Profesa Eliningaya Kweka amesema kuwa, wana maabara zenye idhibati ambazo zinamwezesha mkulima kuunganishwa na masoko ya nje na kupambana na umaskini katika kuongeza pato la nchi.
Amesema kuwa , wanatumia teknolojia bora na za kisasa pamoja na mabomba ya kunyunyuzia viautilifu sambamba na kutumia ndege nyuki kunyunyuzia dawa.
“Tunapenda katoa rai kwa wakulima endapo wakikutana na viuatilifu ambavyo havina nembo kutoka mamlaka hiyo wasitumie kwani zitawaletea shida kwenye afya zao hivyo nawaomba sana wawe makini katika hilo. “amesema Profesa Kweka.