Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP walipomtembelea na kufanya mazungumzo katika Ofisi yake Jijini Dodoma
Mwakilishi Mkazi wa programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya AFDP nchini Bw. Robson Mutendi akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi walipokutana naye Mei 9, 2023 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (mwenye suti ya blue) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Programu ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi ya AFDP walipomtembelea na kufanya mazungumzo katika Ofisi yake Jijini Dodoma Mei 9, 2023.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na; Mwandishi Wetu-Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amekutana na ujumbe kutoka Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya AFDP pamoja na Wataalam na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma Mei 9, 2023.
Katika Mazungumzo yao, Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alieleza kuwa Serikali tayari inatoa ushirikiano wa hali ya juu katika kutekeleza program hiyo na pia, kwa wakati inaainisha masuala mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika utekelezaji wake na kutafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu za Serikali.
Kwa Upande wake, Mwakilishi Mkazi wa program hiyo nchini Bw. Robson Mutendi alisema,ujumbe huu maalum wa ukaguzi wa maeneo ya mradi, utatembelea katika baadhi ya maeneo ambayo mradi unatekelezeka ikiwa ni njia mojawapo ya kuona na kuainisha maeneo yenye mapungufu, ili kufanyiwa kazi na kufikia malengo, na kuomba ushirikiano katika utendaji ili uweze kuleta matokeo tarajiwa.
Baada ya mazungumzo hayo mahususi na Katibu Mkuu, Ujumbe huo pamoja na wataalam utakutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi na pia utambelea baadhi ya maeneo inapotekelezwa program hiyo ikiwa ni pamoja na mikoa ya Tabora, Geita , Lindi na Zanzibar.