MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu Mei 8,2023,amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.8 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),wilaya ya Ikungi.
Vifaa hivyo ambavyo ni gypsum board 75 na rangi ndoo tano vimekabidhiwa mbele ya Kamati ya Siasa ya wilaya.
Akikabidhi vifaa hivyo Mtaturu amesema nia yake ni kuona jengo hilo linakamilika kwa wakati ili Chama kiendelee kutoa huduma kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.
“Viongozi wetu wa Chama wanahimiza kufanya siasa na uchumi ,na kupitia hotuba zao mara kwa mara wanahimiza chama ngazi zote kuweza kujitegemea kiuchumi,nikiwa mmoja wa wanachama na mbunge wa jimbo mojawapo lililopo katika wilaya hii nimeona ni vyema niunge mkono chama change,”,
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya kamati ya ujenzi,Mwenyekiti wa kamati Ally Mwanga amesema wanatambua juhudi za wabunge katika ujenzi huo.
“Nikushukuru sana Mbunge wetu Mh Mtaturukwak uendelea kuchangia ujenzi huu mpaka hapa ulipofikia,kamati itaendelea kujipanga ili kukamilisha ujenzi na vitega uchumi kwa manufaa ya chama,”amesema.
Kwa upande mwenyekiti wa CCM wilaya Mika Likapakapa ametoa shukrani zake kwa niaba ya chama.
“Mh Mtaturu ahsante sana,umeendelea kutoa mchango kwenye ujenzi wa jengo hili la CCM wilaya,kata na matawi,hatua hii inaimarisha chama,”ameshukuru.
Ameelekeza kamati ya ujenzi kujipanga kukusanya nguvu zaidi kumalizia ujenzi huo na vitenga uchumi vya chama.
Juni 15,2021,Mtaturu alishiriki uzinduzi wa ujenzi wa ofisi hiyo ambayo hadi kukamilika kwake inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 152 ambapo ramani yake inahusisha ofisi za jumuiya zote tatu,ukumbi wa mikutano na vyumba vya biashara.
Katika uzinduzi huo alichangia bati 100 na saruji mifuko 100 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5.9.