Waziri wa jinsia wazee na watoto,Dkt Dorothy Gwajima akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha.
……
Julieth Laizer ,Arusha
Waziri wa Jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima amezitaka asasi za kiraia za Afrika Mashariki kuandaa mikakati ya wazi ya ushirikishwaji wa wazi kuhusu masuala ya wananchi ili kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika ngazi za kikanda.
Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa asasi hizo kutoka nchi Saba za Afrika Mashariki unaofanyika mkoani Arusha ambapo ndipo makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki .
Dkt Gwajima amesema maendeleo yoyote huwa hayakosi changamoto hivyo kwa mujibu wa ripoti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekutana na changamoto na zipo katika safari ya kuifikia agenda 2030 ambapo amesema hali ya chakula ilidorora kutokana na Mtikisiko wa Uvico 19.
Naye Mwakilishi wa mkuu wa mkoa ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha Blandina Nkini amewataka washiriki wa mkutano huo kutumia muda wao kutembelea Vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa huo.
Kwa upande wa washiriki wa mkutano huo Adamsoni Nsimba, Emmanuel Nzeyimana kutoka Uganda,wamesema wanatarajia baada ya mkutano huo watakuwa na mikakati mizuri katika kuendesha asasi hizo ikiwa ni pamoja na kuwepo na ukaribu mzuri baina ya Serikali na asasi hizo.
Mkutano huo umezileta pamoja nchi 7 za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Uganda,Kenya, Sudani Kusini, Rwanda,Burundi na Tanzania na mkutano huo utafanyika Kwa siku tatu mkoani Arusha.