Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Dominicus Lusajo,akiongea katika kikao cha kukaribisha ujumbe huo.
Afisa Mwandamizi wa mahusiano ya Jamii na Usimamizi wa miradi Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo,akieleza ujumbe wa wajumbe wa CDC kutoka Mara jinsi utekelezaji wa miradi ya maendeleo unavyofanyika.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Mkoa wa Mara wakitembelea baadhi ya shule zilizojengwa na Barrick Bulyanhulu wilayani Nyang’hwale.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Mkoa wa Mara wakitembelea baadhi ya shule zilizojengwa na Barrick Bulyanhulu wilayani Nyang’hwale.
Baadhi ya Wajumbe waliopo katika ziara hiyo wakisikiliza taarifa ya utekelezajiwa miradi
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Mkoa wa Mara wakitembelea baadhi ya shule zilizojengwa na Barrick Bulyanhulu wilayani Nyang’hwale.
*
Miradi mikubwa iliyofanikishwa na fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, imeweza kuboresha maisha ya Wananchi wengi, kufanya maeneo yenye miradi hiyo kuvutia zaidi pia kuwa mfano wa kujifunza usimamizi na utekelezaji miradi kwa ufasaha.
Wiki hii wilaya ya Nyang’hwale iliyopo wilayani Geita, imetembelewa na viongozi kutoka mkoani Mara, ukiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Dominicus Lusajo, ambaye ameongozana na Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) kwa ajili ya kuona na kujifunza jinsi Barrick Bulyanhulu inavyoweza kufanikiwa kutekeleza miradi ya CSR kwa ufanisi mkubwa ili watumie maarifa hayo kufanikisha zaidi miradi inayotekelezwa na fedha za CSR zinazotolewa na Mgodi wa North Mara.
Afisa Mwandamizi wa mahusiano ya Jamii na Usimamizi wa miradi Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, alieleza ujumbe huo wakati wa kutembelea miradi iliyotekeleza Nyang’hwale kuwa katika kipindi cha 2022 na 2023 Barrick Bulyanhulu imeweza kujenga zaidi ya zahanati 15 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale pia imeweza kujenga na kuboresha miundombinu ya shule na barabara.
Baadhi ya miradi mikubwa iliyojengwa kupitia fedha za CSR za Barrick Bulyanhulu ambayo inaendelea kuleta manufaa kwa Wananchi ni Chuo cha Ufundi Stadi cha Bugarama,Hospitali ya Bugarama,Shule ya Wasichana ya Bulyanhulu,Chuo cha Mafunzo ya Afya cha Ntobo,Kituo cha mabasi cha Segese,Shule ya awali na msingi ya mchepuo wa Kingereza ya Kharumwa ikiwemo pia miradi ya maji safi na barabara.
Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Dominicus Lusajo, akiongea kwa niaba ya viongozi wake,alipongeza kampuni ya Barrick kwa kufanikisha miradi ya maendeleo hususani katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.
Alisema kupitia ziara hii wataweza kujifunza jinsi ya kuibua miradi yenye tija na kuisimamia kwa ufasaha.
Kwa upande wake,Katibu Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale,Husna Toni,alisema kuwa miradi mingi iliyotekelezwa na Barrick ambayo ina ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imeleta maendeleo na inaendelea kuwanufaisha Wananchi.