Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mei 3,2023 jijini Arusha.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Jihn Jingu ,akizungumza wakati akifungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mei 3,2023 jijini Arusha.
Mwenyekiti wa AZAKi za Afrika Masharika Daniel Lema,akizungumza wakati akifungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mei 3,2023 jijini Arusha.
Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani),wakati akifungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mei 3,2023 jijini Arusha.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,lililofanyika leo Mei 3,2023 jijini Arusha.
Na WMJJWM, Arusha
Asasi za kiraia zimetakiwa kuhakikisha shughuli wanazofanya zinalenga kuwanufaisha wananchi hadi ngazi ya chini.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito huo akifungua Kongamano la kwanza la Asasi za Kiraia (AZAKi) za Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jijini Arusha Mei 03, 2023.
Mhe. Dkt. Gwajima amebainisha kuwa, ushiriki wa watu kupitia AZAKi ni muhimu kuhakikisha sera zinafanya kazi hadi mashinani na nafasi muhimu ya Asasi za Kiraia kwenye utafiti, mijadala na kufanya mikutano ya hadhara kuhusu masuala muhimu kwa wananchi.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kukuza ushirikiano na asasi zisizo za kiserikali ili kutunga sera zinazonzingatia mahitaji ya watu na kukuza ukuaji wa uchumi wa jamii ndadani ya kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki”. amesema Dkt. Gwtajima na kuongeza kuwa. “Ni matumaini ya Serikali kuwa, mkutano huu utaandaa viashiria vya wazi vya ushirikishwaji ili kuhakikisha ushiriki mahiri wa AZAKi kama sauti ya wananchi katika ngazi ya kikanda”. Amefafanua Waziri Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima ameongeza kwamba, licha ya mambo mbalimbali ya AZAKi ndani ya nchi washirika, jumuiya imeendelea kuhamasisha ushiriki wa Asasi za kiraia na jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuhakikisha sauti za wananchi wa Afrika Mashariki zinawasilishwa na kuzingatiwa wakati wa kufanya maamuzi.
Aidha amesema anaamini Mkutano huo utawezesha AZAKi kuonesha mafanikio na programu zenye matokeo katika kanda na kuja na matarajio ya wananchi kwa kujikita kwenye mada kama vile za Afya, Utawala na Demokrasia, Biashara na Uwekezaji, Amani na Usalama, Kilimo, Mabadiliko ya Tabianchi, ushiriki wa Jinsia na Vijana ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kijamii na kukuza ustawi wa raia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa AZAKi za Afrika Masharika Daniel Lema amebainisha lengo la kongamano hilo ni kuibua mijadala ya kendeleza utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na watu wake kwa manufaa ya pamoja.
“Kiu ya Asasi hizi ni kuwa sehemu ya juhudi za kuendeleza Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hili litawezekana kama kutakuwa na ushirikiano imara kati ya AZAKi na Serikali za Jumuiya ya Afirika Mashariki” amesema Lema.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa AZAKi za Afrika Mashariki kutoka nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Sudani Kusini, Kenya na Uganda.