KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 2, 2023 jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya maonyesho ya sita ya Mifuko na Programu za Uwezesahaji nchini yanayotarajia kuanza Mei 21 hadi 27 mwaka huu Mkoani Kigoma.
MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF, Bi.Justina Mashiba,akizungumzia maandalizi ya maonyesho ya sita ya Mifuko na Programu za Uwezesahaji nchini yanayotarajia kuanza Mei 21 hadi 27 mwaka huu Mkoani Kigoma.
Mtaalamu wa TEHAMA kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw.Peter Lwanda,akizungumza kuhusu maandalizi ya maonyesho ya sita ya Mifuko na Programu za Uwezesahaji nchini yanayotarajia kuanza Mei 21 hadi 27 mwaka huu Mkoani Kigoma.
Na.Alex Sonna-DODOAM
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya sita ya Mifuko na Programu za Uwezesahaji nchini yatakayofanyika mkoani Kigoma.
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 2, 2023 jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya maonyesho yanayotarajia kuanaza Mei 21 hadi 27 mwaka huu.
“Washiriki katika maonesho haya ni Mifuko na programu za uwezeshaji,Wizara, Taasisi, Mamlaka na Wakala wa Serikali, wafanyabiasahra, Wajasiriamali,Asasi za kiraia, Taasisi za fedha, Elimu na utafiti”amesema Bi.Beng’i
Hata hivyo amewakaribisha wananchi wote wa Kigoma,mikoa jirani na watanzania kwa ujumla kuhiudhuria na kujionea mifuko ya uwezeshaji inavyosaidia kuwawezesha wananchi kiuchumi pamoja na programu zake kwani hakuna kiingilio
Aidha Bi.Beng’i amesema kuwa jumla ya sh.Trilioni 9 zimeshatolewa ikiwa ni mikopo kwa wafanyakazi kutoka katika mifuko mbalimbali.
”Kiasi hicho cha fedha kimewezesha wafanyabiashara kuendeleza biashara zao lakini pia ni sehemu ya mifuko hiyo kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha wafanyabiashara ili waweze kuboresha na kujikwamua kiuchumi.”amesema
Pia ameeleza kuwa jumla ya wananchi milioni 16 wamefikiwa na ajira kutoka katika mifuko hiyo.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF, Bi.Justina Mashiba,amesema kuwa wanaungana na mfuko huo katika maonyesho ili wananchi wa vijijini waweze kujifunza zaidi kuhusu mfuko huo.
”UCSAF watahakikisha kuwa hakuna mtanzania atayebaki nyuma katika suala zima la Mawasiliano”amesema Bi.Mashiba