Na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi
Askari wa Jeshi la Polisi wa vyeo mbalimbali wa Makao Makuu ya Polisi Dodoma leo Aprili 26,2023 wameshiriki zoezi la upandaji miti katika maeneo ya viwanja vya kambi ya Polisi iliyopo Medeli kata ya Chadulu Jijini Dodoma.
Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika ili kuungana na wananchi wote wa Tanzania katika kuazimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Upandaji miti utaboresha mazingira ya nchi yetu na kusaidia kudhibiti madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.
Picha na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi