Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala akizungumza na wananchi wa kata ya Pasiansi viwanja vya shule ya sekondari Bwiru wavulana
Baadhi ya wananchi wa kata ya Pasiansi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na kukagua miradi ya maendeleo
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika kata za Kitangiri na Pasiansi ambapo amewataka wazazi, walezi, walimu na viongozi wa dini kuhakikisha wanaripoti na kudhibiti vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto wadogo ili kulinda vizazi na taifa
‘.. Ndugu zangu kupanga ni kuchagua, Matukio ya ubakaji, ulawiti yanaongezeka siku hadi siku tukichagua kukaa kimya tutaharibu taifa ..’ Alisema
Aidha Mhe Masala mbali na kumpongeza Rais Mhe Dkt Samia na Serikali yake kwa hatua wanazochukua, ameitaka jamii kutochagua aina ya matukio ya kuripoti na aina ya watoto wa kuwasaidia kwa kuwa watoto wote ni mali yao
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Ilemela Ndugu Said Kitinga amewataka wananchi kutumia ofisi yake kwaajili ya kuwasilisha changamoto mbalimbali wanazozipata pindi wanapofuata huduma katika ofisi zilizo chini ya ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo
Nae mwakilishi wa mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni mganga mkuu wa wilaya hiyo Daktari Samson Marwa amewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Marburg, ugonjwa wa kipindupindu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sanjari na kusisitiza ushiriki wa zoezi la chanjo ya Surua Rubela kwa watoto na mabinti
Vicent Malinyo kutoka eneo la Bwiru Ziwani ni miongoni mwa wananchi waliopata fursa ya kuwasilisha kero zao kwa mkuu huyo wa wilaya ambapo amelalamikia urasimu unaosababishwa na viongozi wa mwalo huo kwa kuwazuia baadhi ya wavuvi wasivue huku wengine wakiruhusiwa kinyemela kwa kutoa rushwa