Wajumbe wa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (katikati) akiwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda Mhe. Frank Tumwebaze (kulia) na Kaimu Waziri anayeshughulikia Uchumi wa Buluu Kenya Bi. Betsi Njagi (kushoto) wakati wa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde akizungumza åwakati wa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023
Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023
Washiriki wa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023 waliposimama kuuombea mkutano huo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (wanne kushoto) akiwa na ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (wa pili kushoto ) akiwa na Mawaziri kutoka nchi za Uganda, Kenya na Burundi baada ya kumalizika kwa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala tarehe 20 Aprili,2023
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde amezisihi nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuungana na mamlaka zinazoshughulikia viwanda na biashara na takwimu kuhakikisha mchango wa sekta ya uvuvi unaonekana wazi kwenye pato la Taifa la kila nchi.
Mhe. Silinde (Mb.) ametoa wito huo jijini Kampala, Uganda alipofungua Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 20 Aprili,2023 jijini humo.
Amesema suala la mchango wa sekta ndogo ya uvuvi kuonekana mdogo unatokana na ukweli kwamba mazao ya uvuvi yanahesabiwa katika sekta za kilimo na uzalishaji na mazao mengine yakiingizwa katika mnyororo wa thamani wa sekta nyingine.
Akizungumzia ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria Mhe. Silinde amesema uvuvi haramu na uvuvi uliopitiliza unahatarisha uwepo endelevu wa rasilimali za uvuvi na mazalia yake katika Ziwa Victoria na hivyo suala la ulinzi wake lazima litiliwe mkazo.
Amesema taarifa zinasema kuwa idadi ya Samaki aina ya Sangara kwa mfano imepungua kwa asilimia 33 katika muda wa mwaka 2021 na 2022 na kuongeza kuwa nchi wanachama wa LVFO haziwezi kukaa pembeni na kuacha vitendo hivyo vikiendelea kwakuwa vinaathiri mamilioni ya watu ambao maisha yao yanategemea ziwa hilo.
Amesema uvuvi ni miongoni mwa vyanzo vya uchumi kwa nchi zetu na wananchi kwa ujumla, linatoa maji kwa matumizi ya majumbani na kusapoti shughuli mbalimbali za kiuchumi ukiwemo uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji katika nchi zetu
“Ni wazi kuwa sekta ndogo mbili hizi ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi katika nchi zetu zote na mtakubaliana nami kuwa Uvuvi katika Ziwa hilo unatoa ajira, chakula, mapato kwa familia na kuziwezesha familia hizo kuishi pamoja na kuzipatia nchi fedha za kigeni na mapato kwa nchi na hivyo ni lazima kuziangalia kwa umakini,” alisema Mhe. Silinde.
Mhe Naibu Waziri Silinde alitumia Mkutano huo kuipongeza Sekretarieti ya LVFO na nchi wanachama kwa kuunga mkono utekelezaji wa progrmu na miradi ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji.
Pia nchi wanachama wa LVFO na Sekretarieti ya LVFO kuhakikisha hatua za pamoja za kuwalinda Samaki aina ya sangara na rasilimali nyingine zinazopatikana katika ziwa Victoria ziendelezwe na kuimarishwa.
“Ni wazi kuwa kumekuwa na hatua kubwa katika utekelezaji wa maagizo na maelekzo yanayotolewa na Baraza la Mawaziri, hili linonekana wazi kutokana na idadi ya miradi iliyotekelezwa huu ni ushahidi tosha kuwa sekretarieti ya LVFO iko makini katika kutekeleza maagizo yanayotolewa na Baraza la Mawaziri la sekta, nawapongeza sana,” alisema.
Naibu Waziri pia alipongeza Kamati ya Uratibu inayoongozwa na Makatibu Wakuu kwa kuandaa vyema nyaraka za mkutano wao na hivyo kurahisisha kazi ya Mawaziri katika kikao hicho.
Katika Mkutano huo Tanzania ilikabidhi kijiti cha uenyekiti kwa Uganda na kuipongeza kwa kuchukua nafasi hiyo na hivyo kuitakia utekelezaji mwema wa majukumu yake ya kulinda rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria.