Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akiongea na wahitimu wa Chuo cha Ardhi Morogoro wakati wa mahafali ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akipata maelezo ya namna Chuo cha Ardhi Morogoro kilivyojipanga kuboresha majengo yake kutoka kwa Mkufunzi Pius kafefa wakati wa mahafali ya chuo hicho.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Ardhi Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda wakati wa mahafali ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akijaribu ufanisi wa mashine ya kupimia ardhi kabla ya kufungua mahafali ya Chuo cha Ardhi Morogoro.
Na Mwandishi wetu Morogoro
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda ameagiza Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro Chalse Saguda kuhakikisha somo la Maadili linafundishwa kwa wanafunzi wa chuo hicho ili hapo baadae waweze kukabiliana na changamoto ya rushwa iliyogubika sekta ya ardhi Nchini.
Akioneshwa kusikitishwa na vitendo vya rushwa katika Sekta ya Ardhi Nchini Naibu Waziri Pinda amesema ni lazima vyuo vya ardhi vianzishe mtaala wenye somo la maadili ndani yake ili wanachuo hao watakatakapoanza kuitumikia jamii wasiendelee na changamoto ya rushwa inayoigubika sekta hiyo.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo leo wakati wa Mahafari ya 41 ya Chuo cha ardhi Morogoro yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho nakuhudhuliwa na Wahitimu takriban 300 waliofuzu katika fani mabalimbali za sekta ya Ardhi.
‘’Inasikitisha kuona mwananchi anafuatilia hati mwaka mzima au mwananchi kwenda katika ngazi ya Wizara hadi Ikulu kufuatilia Migogoro wakati Wizara ina watumishi kuanzia ngazi ya Mikoa.’’Aliongeza Naibu Waziri Pinda.
Ameonya kuwa malalamiko ya Wananchi hayatakiwi kwenda kwa viongozi wa wajuu wa Serikali kwani wao sio wataalamu wa ardhi masuala ya Ardhi kwani changamoto hizo ni bora zikatatuliwa na wataalam wenye ujuzi katika fani hiyo.
Pinda ameagiza Wakurugenzi katika Wizara yake waangalie uwezekano wa kutumia wahitimu wapya sekta ya ardhi ili wapewe kazi katika miradi yote inayoendelea Wizarani ili kuwajengea uwezo wa kufanyakazi kiufanisi mara watakapopata ajira rasmi.
Akiongelea kuhusu mikakati ya uendelezaji chuo Waziri Pinda amewataka bodi ya chuo hicho kuanza mara moja hatua za ujenzi wa miundombinu mipya hivyo kuwataka kufika Wizarani ili kuwasilisha andiko lao ili hatua zianze kuchukuliwa.
Pinda ameongoza kuwa Chuo hicho kimekuwa na miundombinu ya zamani na hivyo mahitaji ya kupata miundombinu ya kufundishia haiepukiki na kuhaidi kuwa suala hilo wanaenda kulifanyia kazi.
Pinda ameonya tabia ya baadhi ya wataalam sekta ya ardhi kuacha tabia mbaya nakuepuka vitendo vya rushwa akionya kuwa maaana ya rushwa ni kutenda kazi bila kuzingatia matakwa ya kisheria.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Ernest Kianga amesema kwa kuzingatia mwelekeo uliopo wa mahitaji makubwa ya raslimali watu wenye ujuzi na weledi wa juu kitaifa na kimataifa, Chuo kimeandaa Mpango Kabambe unaoonesha mwelekeo wa ukuaji wa taasisi katika kipindi cha miaka ishirini 20 ijayo, yaani 2023 – 2043, mpango huu unaoelenga kukipanua Chuo kimiundombinu ili kuongeza udahili kutoka wanafunzi 496 waliopo sasa hadi kufikia wanafunzi 5250 lakini pia kuongeza idadi ya wafanyakazi itakayongezeka kutoka 45 walipo sasa hadi kufikia wafanyakazi 310 ifikapo mwaka 2043.
Wakati hguo huo rais wa Chuo hicho Bw. Chacha Marwa amewambia wajumbe wa Bodi na Mgeni rasmi katika Mahafali hayo Naibu Waziri Pinda kuwa miundombinu ya Chuo hicho ni ya zamani ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa na maeneo ya nje ya kujisomea hivyo kumtaka kiongozi huyo wa serikali kutatua changamoto hiyo kwa wanafunzi chuoni hapo.