NJOMBE
Serikali ya mkoa wa Njombe imelifanyia kazi agizo la rais kwa kutenga ekari 89 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Building Better Tommorow (BBT)katika kijiji cha Ikang’asi wilayani Njombe ambapo imekusudia kuanzisha msitu wa kilimo cha kisasa cha Parachichi utakaokidhi mahitaji ya soko la kimataifa.Katika eneo hilo serikali imekusudia pia kujenga miundombinu ya usafirishaji zikiwemo barabara na kiwanja kidogo cha ndege ili kurahisisha usafirishaji wa malighafi hiyo kwenda sokoni.
Awali akiweka bayana mpango wa serikali katika kilimo cha parachichi na programu Ilianishwa na rais Samia ya BBT mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa aliyemwakilisha mkuu wa mkoa katika uzinduzi wa kapameni ya kijanisha maisha iliyoanzishwa na taasisi iliyojipambanua katika kusaidia sekta binafsi ya kilimo nchini PASS Trust amesema wamekusudia kufanya mapinduzi makubwa katika kilimo hicho kwasababu mkoa unaingiza pato kubwa kutoka kwenye zao hilo
Kasongwa anasema ili mradi huo uwe na ufanisi wamefungua milango pia kwa wawekezaji kwenda katika kijiji hicho kuwekeza kwasababu kitawekwa miundombinu yote muhimu huku pia akihimiza taasisi za kifedha kuhakikisha zinaona namna ya kuwasaidia wakulima ikiwa ni pamoja na kupunguza riba.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amesema serikali inatambua jitihada zinazofanywa na taasisi ya PASS Trust za kwa wakulima ikiwemo mikopo na kwamba kupitia mradi wa kijanisha maisha kilimo kitapiga hatua na kutunza mazingira.
“Serikali inatambua jitihada hizi na tutakuwa bega kwa bega kusapoti kampeni yenu kwasababu hata kauli mbiu ya mwaka huu ya mwenge inahamaisha kutunza mazingira,alisema Kissa Gwakisa Kasongwa mkuu wa wilaya ya Njombe.
Kufuatia serikali kuomba PASS kuona namna ya kuwekeza pia katika kijiji cha parachichi kinachokwenda kuanzishwa Lupembe ,Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo ya kilimo Ibrahim Kaduma anasema wamepokea kwa mikono miwili wito huo kwasababu ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Kijanisha Maisha yenye dhamira ya kuinua kilimo ambayo inakuwa na matokeo mengi pamoja na kutunza mazingira.
Kuhusu uzinduzi wa kampeni ya “Kijanisha Maisha kwa Uchumi Endelevu” katika uchumi wa mzunguko hakutakuwa na malighafi inayotelekezwa katika uchumi na kwamba wakati umefika kunufaika na kila kinachozalishwa na mkulima kupitia kilimo biashara .
“PASS Trust malengo yake makuu ni uwezeshaji wa kilimo,uvuvi,mifugo , mazao ya misitu na viwanda kupitia huduma za dhamana na mikopo,na taasisi ya kipekee sana tanzania ambayo inatambulika na baraza la taifa la uweshaji wananchi kuchumi,alisema Ibrahim Kaduma mkurugenzi PASS Trust”
Kwa upande wao wakulima ambao wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo akiwemo Steven Mlimbila maarufu Nemes Green Garden na Vitus Chaula mkulima wa mahindi Kutoka Mavanga Ludewa wanasema mafunzo waliyopewa na kampeni iliyozinduliwa inakwenda kuleta matokeo chanya kwa wakulima na uchumi wa mkoa kwasababu wataanza kufanya kilimo bora na chenye tija.
Aidha wakulima hao wamesema ili kufikia malengo ya kampeni ya kijanisha maisha kwa kilimo endelevu ni vyema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa kilimo kuboresha miundombinu katika maeneo ya uwekezaji na masoko ya uhakika ya mazao ili kuepusha hasara kwa wakulima.
Pato la mkoa wa Njombe kwa zaidi ya asilimia 70 linatokana na mazao huku biashara ya mbao,viazi,mahindi na parachichi zikitajwa kuchangia zaidi.