Mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni ametembelea kiwanda cha kuchakata Tangawizi kilichopo kata ya Mnyamba ambacho kwa kiasi kikubwa hutegemewa na wakazi wa eneo hilo ambao wengi wao ni wakulima wa Tangawizi kuuza Mazao yao.
Pia DC Kaslida kwa niaba ya wakazi wa Same amemshukuru Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kuwajali wakulima kuwezesha kuwepo Kwa kiwanda hicho ambacho ni matokeo ya uwezekeza wa ubia baina ya Ushirika wa wakulima wa Tangawizi na Mfuko wa PSSSF.
Amewasisitizia viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji kuwawezesha wakulima kuwa na soko la uhakika, pia wakulima nao kuchangamkia fursa ya uwepo wa Soko la Tangawizi kukuza kipayo chao.