Joctan Agustino-NJOMBE
Ikiwa siku chache zimepita tangu maduka 21 ya jengo la kitega uchumi cha Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM -UWT Wilaya ya NJOMBE yateketee kwa moto ,baadhi ya wafanyabiashara waliyounguliwa mali zao wamekiri kuibiwa na mali na vibaka wakati wa uokozi.
Wakizungumzia tukio hilo wafanyabiashara hao akiwemo Yohana Sanga wanasema janga la moto ambalo chake bado hakijulikana limesababisha madhara makubwa kwao ikiwa ni kuibiwa bidhaa hivyo wanaomba vyombo vya dola kuwasaka pia watu waliyotumia mwanya huo kuwaibia wafanyabiashara.
Kutokana na athari hiyo wameomba taasisi za fedha na serikali kuona namna ya kuwashika mkono katika kipindi hiki kigumu ili kuwainua tena katika biashara zao.
“Kwa kweli moto huu umesababisha madhara makubwa ,umeunguza mali lakini wakati tunapambana kuokoa malia na kuzima moto bado kuna watu wasiyo na nia njema wametumia mwanya huo kutuibia hivyo tuombe jeshi la polisi kuwatafuta watu hawa na hatua za kisheria zichukuliwe,alisema Yohana Sanga mfanyabiashara katika jengo la kitega uchumi la CCM-UWT NJOMBE.
Ukiachana na athari zilizowakuta wafanyabiashara ,moto huo uliunguza pia gari la mizigo lenye nambari za T936-CDV Scania ambalo lilishika moto upande mmoja baada ya kuegeshwa jirani na duka linalodaiwa kuwa ndiyo kiini cha moto likisubiri kushushwa mzigo.
Dastani Mgaya ambaye ni utingo wa gari hilo la mizigo na Amiri Kihombo ambaye ni dereva wamesema wameathirika vibaya na moto huo kwasababu gari limeungua vibaya na kuhitaji zaidi ya mil 10 kulitengeneza na itachukua zaidi ya wiki tatu kurejea barabarani hivyo wanaomba kupatiwa fidia kwa gari lao limeungua likiwa kazini likishusha mzigo.
Wakitaja athari za moto kwenye gari hilo wamesema baada ya kushika moto betri zikaungua,mfumo wa umeme ,kioo cha mbele na pembeni,siti na matairi matatu hivyo wakati wafanyabiashara wakifiriwa kushikwa mkono wanahitaji na wao kupewa fidia kwa kusababishiwa ajali hiyo.
“Wakati tunazima moto tuliona mlinzi akisema wakati amejiegesha kwenye mlango wakibanda akiota moto aliona joto kali linatoka ndani ya kibanda na kisha baadae kuona moshi ukitoa nje hatua ambayo ilimlazimu kuanza kuomba msaada kuwasaidia kuzima moto katika moja ya kibanda na kisha kushika gari lao la mizigo lililokuwa limepaki jirani,alisema Dastan Mgaya ambaye ni utingo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa NJOMBE ERASTO MPETE ameendelea kusisitiza wafanyabiashara kujikinga na visababishi vya matukio ya moto huku katibu tawala wa wilaya ya Njombe Emmanuel George akiwataka wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kukata bima za baiashara ili kuweka mazingira salama mitaji yao endapo wakikutwa na majanga kama hayo.
George alisema walifanikiwa kuzima moto majira ya saaa nane usiku na kwamba tathimini ya awali imeonyesha maduka 21 ndiyo yaliyoathirika na moto hivyo wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha moto na kutazama madhara ya moto huo ili hatua nyingine zichukuliwe.