Naibu katibu Mkuu, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Ally Poss, akizungumza na wafanyabishara na Watumishi wa Bandari, Wizara , TRC na TRA,(Hawapo pichani) katika kuboresha utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki ambao ni wafanyabishara na Watumishi wa Bandari, Wizara , TRC na TRA, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Sekta ya Uchukuzi, Dkt Ally Possi,(Hayupo pichani), katika kikao cha kuboresha utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam.
Na.Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM
Naibu katibu Mkuu Sekta ya Uchukuz, Dkt Ally Possi amezitaka taasisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Reli (TRC) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wanaweka Mazingira Rafiki kwa wafanyabiashara ili kuanza kutumia Bandari kavu ya kwala kwani kwasasa ujenzi wa Bandari hiyo umefikia asilimia 98.
Possi ameyasema hayo kwenye kikao kilichowakutanisha wafanyabishara wa Bandari, Wizara , TRC na TRA, katika kuboresha utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam.
“ Ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala umefikia asilimia 98 hivyo taasisi zote zinatakiwa ziwezeshwe kuhamia ili kupunguza Msongamano wa Mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam” alisema Dkt.Possi
Aidha, Dkt. Possi amezielekeza taasisi hizo kutoongeza gharama katika kusafirisha Mizigo kutoka Bandari ya Dar es Saalam Mpaka kwala, kwani kuongezeka kwa gharama kutaongeza wafanyabiashara kutotumia bandari hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara katika sekta ya Bandari wamesema kuwa wapo tayari kutumia Bandari ya Kwala kwani bandari hiyo itasaidia kupunguza Mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, hivyo wanaomba Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), kuendelea kusimaia mifumo ya utoaji huduma ili kusiwe na usumbufu. .
Naye Meneja Uendeshaji kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani amesema tayari Shirika hilo limeshatenga Mabehewa pamoja na vichwa vya treni kwa ajili ya kuanza kusafirisha Mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Kwala.
Kwa upande wake Meneja Msimamizi wa Ujenzi wa Bandari hiyo Alexander Ndibalema amesema kuwa ujenzi wa miundombinu ya reli na Barabara ya Kilometa 15 kutoka Vigwaza mpaka Kwala umekamika hivyo Bandari hiyo ipo tayari kuanza kazi.