Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Marburg.
…………………..
NA MUSSA KHALID
Wizara ya Afya imesema jumla ya watu 212 waliotangamana na wagonjwa wa Marbug wamebainishwa huku yao, watu 35 wamemaliza siku 21 za uangalizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa huo na kuruhusiwa kutoka katika karantini na kurejea kwenye familia na shughuli zao.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Marburg ambapo amesema hadi kufikia leo jumla ya visa nane na kati ya yao watano wamefariki na mmoja amekiwa tayari ameruhusiwa na wawili wakiendelea na matibabu.
Amesema serikali inaendelea kuwahakikishia watanzania na jamii ya Kimataifa kuwa Tanzania ni salama dhidi ya ugonjwa wa Marburg uliogundulika Bukoba mkoani Kagera hivi karibuni.
“Nisisitize tena kwamba, endapo kutakuwa na mtu yeyote kwenye jamii mwenye dalili za homa kali, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu, tutoe taarifa haraka kwa kupiga simu 199 bila gharama ili Pia kupata msaada wa wataalam haraka na kuchukua hatua zinazostahili”amesema Waziri Ummy
Waziri Ummy amewahimiza wananchi wote hasa wa Mkoa wa Kagera kuendelea kuchukua tahadhari ya kudhibiti na kuzuia maambukizi mapya katika jamii.
Waziri Ummy amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hata pale mgonjwa wa mwisho kupona atakaporuhusiwa hawana budi kuendelea kuchukua tahadhari hadi watakapojiridhisha kwamba ugonjwa umeisha.
Hata hivyo amewakumbusha watumishi wa afya kote nchini kuendelea kuimarisha afua za kujikinga katika vituo vyote nchini na kuzingatia kanuni za afya za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza (IPC) wakati wote wa kutoa huduma.